![]() |
| Michael Jackson (kushoto) akiwa na Ola Ray katika "Thriller". |
Shilingi milioni 88 ... hiki ndicho kiasi alichotaka msichana kutoka kwenye video yake ya muziki ya "Thriller" ya Michael Jackson ili kuweza kusimamisha vita na wakala wa mfalme huyo wa miondoko ya Pop, imefahamika.
Ilivujishwa habari kuwa Ola Ray ameafikiana katika mashitaka yake na wakala huyo mapema mwaka huu, na sasa inafahamika kwamba ... Shilingi milioni 88 zitakwenda kwa Ola na Shilingi milioni 32 atalipwa mwanasheria wake.
Ola alifungua madai dhidi ya wakala wa Michael Jackson na kampuni yake ya uzalishaji mnamo Mei 2009 -- mwezi mmoja kabla ya kifo cha Michael Jackson -- akilalamikia kuvunjwa kwa mkataba. Ola alisema alikuwa bado anadai kitita kinene kutoka katika faida ya "Thriller" ... karibu miaka 30 baada ya kuwa imeingizwa sokoni.
Mwongozaji wa video hiyo ya muziki, John Landis -- ambaye alifungua madai yanayofanana na hayo dhidi ya wakala huyo -- naye pia amefikia mwafaka ... lakini anataka kulipwa Shilingi bilioni 3.2 zaidi.

No comments:
Post a Comment