Saturday, January 5, 2013

MWANAMITINDO NAOMI CAMPBELL SASA ATEMBELEA MAGONGO...

Naomi Campbell ameripotiwa kuumia kano katika mguu wake baada ya kuvamiwa kwenye mtaa mjini Paris.
Mwanamitindo huyo alikuwa akiita teksi ndipo aliposhambuliwa na kuporwa na washambuliaji kadhaa, imeripotiwa. Shambulio hilo -- ambalo lilitokea zaidi ya mwezi mmoja uliopita -- limemwacha Naomi akilazimika kutembelea kiti cha magurudumu na magongo.
Taarifa zinasema rafiki wa kiume wa Naomi, Vladimir Doronin, amemwongezea ulinzi wake tangu kutokea tukio hilo.
Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, Naomi alieleza, "Samahani, sizungumzi na vyombo vya habari, lakini mimi ni mzima."

No comments: