![]() |
| Cameron akionesha fizi zake tupu mbele ya mama yake, Wendy Jackson. |
Mtoto wa kiume mwenye miaka mitano ambaye aling'olewa meno yake 13 ya utotoni baada ya kuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya meno amekubali fidia ya Pauni za Uingereza 9,000 kutoka kwa daktari wake wa meno.
Cameron Jackson alibakiwa na meno saba tu hadi atakapofikia umri utu uzima baada ya meno yake yaliyooza kuondolewa miaka miwili iliyopita.
Mama yake, Wendy Jackson, mkazi wa Bradford, West Yorkshire, alichukua hatua za kisheria dhidi ya daktari wa meno, Dk. Raymond Matloa na sasa amekubali fidia ya Pauni za Uingereza 9,000 ili kumaliza suala hilo nje ya mahakama, kiasi ambacho Cameron atapokea pale atakapotimiza umri wa miaka 18.
Daktari huyo wa meno, Dk. Raymond Matloa, anayefanya kazi katika zahanati ya Fountain Street Medical Practice iliyoko Morley, hajakubali kuhusika na kosa la upotevu wa meno ya Cameron.
Wendy mwenye miaka 31, alisema kila mara alikuwa akimpeleka Cameron kwa ajili ya uchunguzi na kusafisha meno yake lakini maumivu ya meno yake yakazidi kuwa makali.
"Alikuwa akipata unafuu wa maumivu kila ifikapo usiku sababu alikuwa akiamka usiku na kuanza kulia," alisema.
Mwaka 2010, aliondolewa meno kwa ganzi katika taasisi ya meno mjini Leeds.
Wendy alisema Cameron hawezi kukumbuka upasuaji huo lakini sasa anafahamu vema kuhusu muonekano wake.
Alisema: "Hapendi kutabasamu sababu anahofia kwamba kuna mtu anaweza kusema "Kwanini huna meno?"
Cameron kwa sasa anamudu kula bila meno yake, na pia anaweza kung'ata matunda kwa kutumia fizi zake.
Wendy alisema ameelezea taarifa hiyo kwa mtoto wake kwa kusema ilikuwa kama ziara kutoka kichimbakazi cha meno.
Alisema: "Nafurahi kwamba hili limetatuliwa na tunaweza kuanza kusonga mbele.
"Cameron anaendelea vizuri mno na amekuwa jasiri kuhusu kila kitu, jambo tunaloshukuru mno."
Mwanasheria wa familia, Heather Williams alisema meno ya ukubwani ya Cameron yataota atakapokuwa mtu mzima.
Alisema: "Japo ni meno ya utotoni ambayo Cameron amepoteza, itabaki hivyo kwa miaka michache kabla meno yake ya ukubwani kuchomoza. Kwa wakati huu, atalazimika kushughulika na meno machache kuliko inavyotakiwa - kitu ambacho hakuna yeyote angependa kupitia, hasa katika umri wake."
Haifahamiki kwanini meno ya Cameron yalianza kudhoofika alipokuwa na umri wa miezi 18 tu, lakini mama yake alisisitiza hakuwa akila pipi wakati ilipoanza hali hiyo.
Alisema alianza kumpeleka mtoto wake kwa ukaguzi wa kawaida wakati akiwa na umri wa miezi tisa.
Wendy alisema: "Kwanza nilianza kugundua kuna tatizo pale Cameron alipokuwa akishindwa kula vyakula vigumu akiwa na umri wa miezi 18. Alishindwa kula vyakula vigumu kabisa na hakuweza kugusa pipi. Alikuwa akinywa tu maziwa.
"Wakati ndugu yake, ambaye wakati huo alikuwa na mwaka mmoja, alikuwa akila vyakula na Cameron aliweza tu kunywa maziwa nikajua kuna tatizo. Daktari wake wa meno aliendelea kusema meno yake hayana tatizo lakini japo niliweza kuona yalikuwa ya njano, sio meupe kama maziwa meno yanavyotakiwa kuwa.
Alisema: "Mwanzoni daktari wa meno alisema alikuwa akila mno pipi, ambapo nilijua haikuwa sahihi sababu Cameron hakuwahi kugusa chakula chochote kigumu, achana na pipi.
"Kisha nikashauriwa kubadili chupa yake na kutumia kikombe kupunguza mgandamizo katika fizi zake.
"Pia nilimpeleka kwa daktari wake lakini akasemekana hakuwa na tatizo.
"Sifahamu kilichombadili mawazo yake lakini Desemba 2010, wakati akiwa na miaka mitatu, daktari huyo wa meno alimhamishia Hospitali ya Rufaa ya Leeds.
"Mwanzoni walisema lazima nilitumia kitu fulani wakati nikiwa mjamzito kilichosababisha kuoza kwa meno na kuulizwa kama kuna dawa zozote anazotumia.
Wendy anasema ameachwa bila majibu yoyote ya kwanini meno ya mtoto wake yamekuwa hivyo yalivyo.
Alipofuatwa, daktari wa meno wa Cameron, Matloa alikataa kuzungumzia chochote hiyo jana.

No comments:
Post a Comment