Edo Mwamalala. |
Ziara zinazofanywa na mchumba wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willibrod Slaa, Josephine Mushumbushi ‘kukagua uhai’ wa chama hicho mikoani, zimeleta msuguano ndani ya chama , huku wasemaji wakikwepa kutoa ufafanuzi.
Jana aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Edo Mwamalala, alidai kuwa Josephine anafanya ziara mikoani kwa gharama za chama na kuhoji yeye ni nani ndani ya Chama hicho.
Mwamalala aliyejiuzulu unachama wa Chama hicho Januari 3 mwaka huu, alisema hayo Dar es Salaam alipokuwa akitangaza kujiunga rasmi na Chama cha NCCR-Mageuzi.
Mwamalala alidai, inashangaza kuona baada ya Dk Slaa kutangaza nia ya urais, mchumba wake Josephine amekuwa akifanya ziara katika mikoa mbalimbali wakati haifahamiki nafasi aliyonayo ndani ya Chadema mbali ya kuwa mwanachama wa kawaida.
“Je, huyu ni ‘First Lady’ (mke wa Rais) au nani? Hali hii inakivuruga chama ilihali inafahamika wazi kuwa Chadema wamekuwa wakipinga kwa nyakati tofauti mke wa Rais kufanya ziara mbalimbali nchini.
“Kama si ubadhirifu wa fedha na utoaji wa posho kinyemela ni nini? Ukihoji wanadai umehongwa, umetumwa, pandikizi au masalia lakini haya ni matumizi mabaya ya fedha,” alisema.
Akijibu tuhuma hizo, msemaji wa Chadema John Mnyika, alisema si kweli kuwa anatumia fedha za Chama hicho kama ilivyodaiwa na Mwamalala na zaidi alidai kuwa hizo ni propaganda zinazotolewa ili kuchafua chama hicho.
“Nina ushahidi kuwa Mwamalala alikuwa kibaraka aliyetumwa na CCM ndani ya Chadema ili kukivuruga chama na tuhuma zote alizozitoa hazina ukweli, huyo ni mamluki aliyefukuzwa na wanachama baada ya kuonekana hafai,” alisema Mnyika.
Hata hivyo alipotakiwa kueleza ni wapi Josephine anatoa fedha za kufanya ziara hizo, alisema hayuko tayari kumzungumzia mtu zaidi atafutwe mhusika ili atoe ufafanuzi suala hilo mwenyewe huku akikataa kutoa namba ya simu ya Josephine.
Naye Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene, alisema yeye pamoja na Chama chake hawamtambui Mwamalala isipokuwa huo ni muendelezo wa matukio yanayofanywa na baadhi ya watu kukichafua chama hicho.
Mwamalala aliendelea kudai kwamba vitendo vya ukiukwaji wa Katiba na kanuni ndani ya Chadema, ukabila, udini, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ubabe wa uongozi wa chama hicho Taifa, ni miongoni mwa mambo yaliyomchosha na kuamua kuhama.
Pia alihoji utaratibu wa kila mwezi wa Chadema kumlipa Dk Slaa posho ya kujikimu Sh milioni 7. Hata hivyo utaratibu huo umewahi kutolewa ufafanuzi kuwa ni makubaliano yaliyofikiwa ili Dk Slaa aache ubunge, aimarishe chama.
Lakini Mwamalala aliendelea kuhoji: “Ndani ya Chadema utakapotofautiana kimtazamo au kimawazo na Mbowe (Freeman, Mweyekiti) au Dk Slaa katika masuala ya msingi ya ujenzi wa chama, utasemwa umehongwa, umetumwa au wewe ni pandikizi la CCM.”
Alidai hali inavyoonekana, viongozi hao wanapenda sera za CCM zidumu katika mawazo yao na ishara ya suala hilo ni pale wanapofanya mambo kinyume na masuala wanayoyapinga kila siku katika matamshi yao.
Alisema ameamua kujiunga NCCR-Mageuzi na kutamba kuwa huo ni mwanzo tu, yeye ametangulia na anaamini kuna wengi watakuja au kufuata hatua kwa hatua.
Kuhusu Dk Slaa kumiliki kadi ya CCM, alisema imedhihirisha kuwa yeye ndiye masalia ndani ya chama hicho na siyo wale ambao wamekuwa wakituhumiwa na kufukuzwa mara kwa mara bila kutumia utaratibu wa vikao ambao ndio wa kidemokrasia.
Pia alisema haingii akilini kwa Watanzania kumuona Mbowe akiendelea kulitumia gari la Serikali kwa nafasi yake ya Kiongozi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati aliwahi kusimama bungeni na kudai kuwa kitendo cha Serikali kununua magari ya kifahari yenye thamani ya Sh milioni 300 ni matumizi mabaya ya fedha.
Alidai kauli hiyo na zingine ndizo zinazotumiwa na Chadema kuipaka Serikali matope na kueneza uongo kwa Watanzania huku kikiwadhalilisha wanachama na viongozi wa chama hicho.
Naye Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, Moses Machari, aliyemkabidhi Mwamalala kadi ya Chama hicho, alisema hivi sasa Tanzania inapita katika kipindi kigumu katika siasa, kutokana na uwepo wa viongozi wengi wanaozushiana uongo na uropokaji.
Alisema ni vyema watu hao wawe na fikra zitakazowaunganisha wananchi wao ili kuwatendea haki baada ya wao kuwapa dhamana ya kuwaongoza.

No comments:
Post a Comment