KUSHOTO: Mabaki ya mejengo yaliyobomoka baada ya shambulio hilo la bomu. KULIA: Msichana Baraa akipatiwa huduma baada ya kufukuliwa kwenye kifusi alimokaa kwa masaa 11. |
Msichana ambaye alifukiwa kwa masaa 11 chini ya jengo lililolipuliwa kwa bomu nchini Syria alitolewa kwenye kifusi akiwa hai kimiujiza huku akiwa na majeraha kadhaa madogo.
Baraa, ambaye nina lake linamaanisha 'Isiyo na hatia' katika Kiarabu, alifukuliwa na majirani zake akiwa na mikwaruzo, kuvilia damu, kutokwa damu puani na kuvunjika mkono.
Yeye na mama yake wanaishi mjini Daraya, mji ulioko kusini mwa Damascus ambao umekuwa ukikabiliwa na mapigano makali kati ya vikosi vya Rais Bashar al-Assad na wapiganaji wa majeshi ya waasi kwa ajili ya taasisi za serikali na uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko mjini humo.
Majeshi ya Assad yametumia wiki kadhaa kujaribu kuwaondoa wapiganaji wa Chama cha Upinzani cha Wakurdi wa Syria ambao wanaendesha harakari zao kwa kificho mjini humo.
Baraa na mama yake waliamua kujificha pale waliposikia majeshi ya Assad yalikuwa yakisonga mbele, na wao na watu wengine 29 - wakiwamo ndugu zake watatu - wakatafuta maficho chini ya jengo moja mjini humo.
Kwenye video iliyotumwa na wanaharakati wa upinzani katika mtandao wa YouTube, aliwaeleza madaktari: "Watu fulani walitueleza kwamba muundo wa jengo hilo haukuwa imara kihivyo. Lakini tukaa hapo kwa siku tatu."
Baada ya masaa 36 mashambulio ya roketi, ndege za kivita za serikali zilifunika anga la mji huo na kudondosha mabomu kwenye hifadhi ya Baraa.
Alisema: "Kitu cha mwisho nilichokiona kilikuwa mwale mwekundu kama moto. Baada ya hapo likawa giza totoro.
"Nilikuwa nikipumua kwa shida mno."
Mama yake Baraa alinusurika, lakini jamaa zake wenye umri wa miaka 11, tisa na miwili wote walifariki katika shambulio hilo.
Msichana huyo baadaye alitibiwa na madaktari maalimu, ambao walionekana kwenye video wakiondoa kifusi kutoka kwenye pua yake na kooni.
Kwa mujibu wa mtandao wa upinzani Kamati ya Uratibu nchini Syria, watu 183 walifariki katika vita Ijumaa, na wengine 70 juzi asubuhi.
Mapigano hayo yanaendelea huku viongozi wa upinzani wakiwa wamezindua awamu ya pili ya azma yao kuunda serikali ya mpito.
Inaaminika makubaliano kati ya wajumbe 70 wa Muungano wa Kitaifa, kundi mwavuli la Wapinzani nchini Syria likijumuisha magharibi na ghuba, linaweza kusaidia kufikisha ujumbe wa shaka ya kimataifa kuhusu kukosekana umoja miongoni mwa taasisi hiyo.
Umoja wa Mataifa unakadiria watu 60,000 wameuawa nchini Syria katika miezi 22 ya mzozo huo.
Katika mauaji ya halaiki ya hivi karibuni, zaidi ya wanaume wa Sunni 100, wanawake na watoto walishambuliwa katika wilaya inaoshikiliwa na wapinzani katika jiji ya Homs Jumanne iliyopita, kwa mujibu wa wanakampeni wa upinzani.
Mauaji hayo yametokea takribani muda huo huo wa shambulio la ushindani lililoua na kujeruhi mamia ya watu katika Chuo Kikuu cha Aleppo, kitovu cha maandamano ya amani wakati wa kuanza vuguvugu hilo la kudai mabadiliko.

No comments:
Post a Comment