![]() |
| Wanakijiji wakimsulubu Mbunge huyo wa chama tawala. |
Mwanasiasa anayeongoza nchini India amepokea kipigo kikali baada ya kudaiwa kumbaka mwanamke ndani ya nyumba yake usiku wa manane.
Mbunge huyo wa Assam kupitia chama tawala cha Congress, Bikram Singh Brahma, alidaiwa kumbaka mwanamke katika kijiji cha Santipura kilichoko kwenye wilaya ya Chirang jimboni humo kabla ya kukamatwa na wanakijiji jana.
Hili ni tukio jingine la kushitusha la udhalilishaji wanawake katika nchi ambayo inajaribu kujisafisha kufuatia kubakwa na kundi la wahuni na kufariki mwanafunzi mwenye miaka 23 wiki iliyopita, ambapo wanaume watano wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
"Watu walitoa taarifa usiku wa kuamkia jana baada ya kiongozi wa Congress, Bikram Singh Brahma kudaiwa kumbaka mwanamke," mkuu wa polisi wa Chirang Kumar Sanjeev Krishna alieleza.
Inasemekana alikwenda kutembelea kijiji hicho cha Santipur katika mpaka wa Bhutan ndipo akaingia nyumbani kwa mwanamke huyo na kumbaka.
Brahma, ambaye ni mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa chama cha Congress katika wilaya ya Baksa na Mratibu wa chama hicho katika Halmashauri ya wilaya ya Bodoland, kisha alipigwa na wanaume na wanawake ambao walimchania nguo zake.
Hatimaye baadaye alikabidhiwa kwa polisi ambao walimkamata, alisema Krishna.
Waziri Mkuu Tarun Gogoi, alisema yeyote anatepatikana na hatia ya makosa ya kuchukiza "hawezi kuvumiliwa, awe ni mbunge au la."
"Ni uamuzi wa kushutumiwa mno. Yeyote ambaye anafanya ubakaji au kujaribu atapewa adhabu kali," alisema, akiongeza serikali yake imekuwa haina huruma katika kushughulikia kesi kama hizo.
Kiongozi wa chama cha Congress, Digvijay Singh amesema endapo Brahma atapatikana na hatia atafukuzwa katika chama hicho.

No comments:
Post a Comment