![]() |
| Hoteli ya Corridor Springs. |
Mgogoro wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati, imeingia katika sura mpya baada ya wafanyabiashara 17 jijini hapa walioshawishiwa kukubali kuokoa mali za Kanisa hilo zisipigwe mnada.
Taarifa za ndani katika Dayosisi hiyo, zimeeleza kuwa uamuzi wa kushawishi wafanyabiashara hao ambao walikubali kunusuru mali za Kanisa zisipigwe mnada, ulifikiwa katika kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi mwishoni mwa mwaka jana jijini hapa.
Awali kabla ya matajiri hao kuingilia kati, moja ya benki za biashara (jina tunalo) iliipa Dayosisi hiyo muda hadi Desemba 31 mwaka jana, iwe imelipa deni la Sh bilioni 11 vinginevyo mali zake zipigwe mnada.
Kutokana na taarifa hiyo ya benki, Kanisa lilitoa waraka wa Askofu ambapo waumini walitakiwa kila mmoja kuchangia Sh 20,000 ili kunusuru mali za Kanisa zilizo hatarini kufilisiwa mwezi huu baada ya hoteli ya Corridor Springs, mali ya Kanisa hilo kudaiwa fedha hizo.
Baada ya waraka huo, baadhi ya waumini akiwamo Mchungaji Philemon Mollel aliyekuwa kiongozi wa Usharika wa Ngateu, walitaka waliohusika na uzembe uliosababisha deni hilo, wawajibike kabla ya waumini kutoa mchango huo.
Waumini hao walikuwa wakimlenga Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazani Kati, Israel ole Karyongi, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hoteli ya Corridor Springs, bodi husika na menejimenti kuwajibika.
Hata hivyo, hatua iliyochukuliwa na kuthibitishwa na Karyongi ni kufukuzwa kwa Meneja wa Hoteli hiyo, John Njoroge ili kupisha uchunguzi wa chanzo cha kulimbikizwa kwa deni hilo. Pia Mchungaji Mollel alisimamishwa kazi.
Katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi, taarifa zilisema ilikubalika iundwe kampuni ya Arusha Lutheran Investment Limited (ALUICO), itakayohodhi mali za Kanisa na iuze hisa kwa wafanyabiashara hao.
Chanzo hicho kilieleza kuwa baada ya kushawishiwa na kugundua thamani ya mali hizo hasa maeneo zinakopatikana kuwa ni kubwa, haraka wafanyabiashara hao walitoa Sh bilioni 1.7 baada ya kila mmoja kutoa Sh milioni 100.
“Kwanza tumeshangaa kuona Kanisa limeamua kufungua kampuni ya kibiashara tofauti na lengo la kuwepo kwake ambako ni kuokoa roho za washarika, hivi tunakwenda wapi?
“Matajiri hao sasa ndio watakaoamua ni kwa namna gani sadaka na zaka za washarika ambazo zilitumika kujenga rasilimali hizo zitakavyotumika, huu ni ufisadi mkubwa kama ufisadi mwingine wowote,” alihoji mtoa habari wetu.
Taarifa zaidi zilisema baadhi ya mali za Dayosisi ambazo hisa zake zimeuzwa kuwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Selian, Corridor Springs, majengo kadhaa yaliyoko jijini hapa na shule za sekondari na ufundi.
“Kila mmoja alioneshwa kupitia kumpyuta katika kikao hicho, mahali mali hizo zilipo na thamani yake na wakashawishiwa kununua kila mmoja hisa zenye thamani ya Sh milioni 100.
“Kwa kuwa mali hizo nyingi ziko maeneo nyeti kibiashara jijini, wengi walikubali papo hapo na hata wengine waliandika hundi wakiwa bado katika kikao hicho kwa kuwa wana uhakika fedha zao ziko salama au vinginevyo watalazimika kuuziwa mali hizo,” alisema mtoa habari.
Wakati huo huo, kikao hicho kiliamua kumwongeza mkataba wa mwaka mmoja Karyongi baada ya mkataba wake wa awali kwisha Desemba 31 mwaka jana. Karyongi alitafutwa kutoa ufafanuzi lakini simu yake iliita bila majibu.

No comments:
Post a Comment