DK MWAKYEMBE AMTAJA HADHARANI 'MCHAWI' WA ATCL...

Moja ya ndege za ATCL.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, amesema Shirika la Ndege (ATCL), limesambaratishwa kwa ufisadi na amegundua kuwa litachelewa kurudi katika hali yake ya zamani.
Amesema baada ya kugundua kuwa itachukua muda  kurejea katika hali yake ya awali, ameshawishi kampuni zingine kutoa huduma za usafiri wa anga nchini kwa bei nafuu.
Akizungumza  jijini Mwanza jana kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na baadhi ya mawaziri, Dk Mwakyembe alisema katika ushawishi huo, ujio wa Kampuni ya Ndege ya Fast Jet, una lengo la kuweka adabu katika utoaji wa huduma hizo.
Alisema kabla ya jitihada hizo za Serikali, gharama ya usafiri wa ndege kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam ilikuwa sawa na nauli ya Dar es Salaam kwenda Dubai katika Nchi za Falme za Kiarabu.
Kuhusu usafiri wa reli, alisema Serikali imeagiza mabehewa 274 mapya na injini mpya 13 ili kuimarisha usafiri huo huku injini nyingine nane zikikarabatiwa hapa nchini.
Alisema pia mabehewa mengine 34 ya breki, mapya yameagizwa kwa ajili ya uimarishaji wa huduma hiyo na kuwataka wanaofanya biashara kando ya reli, kuondoka haraka.
Kuhusu huduma za bandari, alisema baada ya kumaliza kuisafisha Bandari ya Dar es Salaam, yeye na Naibu wake, Dk Charles Tizeba watahamia katika Bandari ya Mwanza kwa kuwa nayo inayo madudu mengi.

1 comment:

Anonymous said...

After getting more than 10000 visitors/day to my website I thought your ziro99.blogspot.com website also need unstoppable flow of traffic...

Use this BRAND NEW software and get all the traffic for your website you will ever need ...

= = > > http://get-massive-autopilot-traffic.com

In testing phase it generated 867,981 visitors and $540,340.

Then another $86,299.13 in 90 days to be exact. That's $958.88 a
day!!

And all it took was 10 minutes to set up and run.

But how does it work??

You just configure the system, click the mouse button a few
times, activate the software, copy and paste a few links and
you're done!!

Click the link BELOW as you're about to witness a software that
could be a MAJOR turning point to your success.

= = > > http://get-massive-autopilot-traffic.com