WAZAZI WA MBAKAJI WAMCHOMA MOTO BINTI ASIENDE KUSHITAKI...

Wanawake nchini India wakiandamana kupinga vitendo vya ubakaji nchini humo.
Balaa la ubakaji nchini India limezidi kukua jana pale ilipobainika mwanafunzi wa kike alifariki wiki mbili zilizopita baada ya mvulana ambaye alijaribu kumbaka kumchoma moto - kwa kusaidiana na wazazi wake.
Binti huyo mwenye miaka 15, kutoka kijiji cha Jigna kilichopo kaskazini mwa India, alikimbizwa hospitali baada ya  shambulio la Januari 6 akiwa na majeraha ya kutisha ya moto yaliyotapakaa asilimia 80 ya mwili wake.
Licha ya madaktari kupambana kwa wiki mbili kuokoa maisha yake, alifariki kutokana na majeraha yake Jumapili.
Polisi wamemfungulia mashitaka Gyan Singh na wazazi wake kwa mauaji kufuatia kifo chake na kusema watu hao watatu wanakabiliwa na adhabu ya kifo endapo watapatikana na hatia.
Ilidaiwa watuhumiwa hao watatu walimmwagia petroli na kumchoma moto sababu walikuwa wakihofia kwamba lazima angeshitaki polisi dhidi ya Gyan ambaye alijaribu kumbaka jana yake.
"Kufuatia kifo cha msichana huyo tuna uthibitisho wa kutosha kushinikiza hukumu ya kifo lwa Gyan na wazazi wake ambao walikamatwa mara moja baada ya msichana huyo kulazwa hospitalini," Mkuu wa Polisi wa Allahabad Mohit Agrawl alisema.
Hili ni tukio la karibuni katika mlolongo wa ubakaji wa kutisha katika miezi ya hivi karibuni ambayo yametikisa India kwa kiwango chake.
La kwanza, Desemba 16 mwaka jana, ilishuhudiwa mwanafunzi wa udaktari mwenye miaka 23 akibakwa na genge la wahuni watano ndani ya basi mjini New Delhi kabla ya kutupwa nje, akijeruhiwa vibaya na kuachwa uchi, kwenye barabara akiwa hana msaada wowote akisubiria mauti.
Siku 13 baadaye alifariki hospitalini. Wanaume wanaodaiwa kumshambulia wanasubiri hukumu kutokana na mashitaka ya kubaka na kuua.
Kumekuwa na maandamano makubwa nchini India tangu wakati huo, na maandamano makubwa zaidid kwa ajili ya haki za wanawake, sheria kali zaidi dhidi ya ubakaji na shinikizo kutaka wabakaji wanyongwe.
Wakati huohuo wiki iliyopita, mahakama maalumu iliyoanzishwa kushughulikia kesi za makosa dhidi ya wanawake imeamuru adhabu ya kifo kwa mwanaume wa miaka 56 kwa kumbaka na kumuua mtoto wa chini ya miaka 18.
Jaji Virender Bhat, ambaye anaongoza mahakama hiyo maalumu iliyoko ndani ya Mahakama ya Dwarka, imetoa adhabu hiyo kali kwa Bharat Singh, mlinzi wa shamba mjini West Delhi.
Pamoja na adhabu ya kifo, mahakama hiyo imeamuru faini ya Rupia 50,000 kwa Singh chini ya kifungu 302 (mauaji) cha Sheria ya Adhabu ya India (IPC).
Januari 15, mamia ya watu walizingira shule katika jiji la Vasco da Gama huko Goa kupinga baada ya msichana wa miaka saba kudaiwa kubakwa kwenye vyoo vinavyopakana na ofisi ya mkuu wa shule hiyo.
Siku moja kabla, wanaume sita walikamatwa baada ya kudaiwa kutokea shambulio jingine baada ya mwanamke kudaiwa kubakwa na genge la wahuni ndani ya basi mjini New Delhi.
Muathirika huyo alikuwa akisafiri kwenda nyumbani kwa wakwe zake mjini Punjab, Ijumaa ndipo anapodaiwa kunaswa na wahuni hao wilaya ya mpakani Amritsar, mji mtakatifu wa Sikh.
Wanaume watano wameungana na dereva na kondakta, ambao walimpakia msichana huyo kwenye pikipiki na kutokomea naye kusikojulikana, na kumgeuzia kibao na kumbaka mwanamke huyo mwenye miaka 29.
Lakini hizi ni kesi chache tu ambazo zimegusa hisia za jamii katika miezi ya hivi karibuni.
Katika 'mji mkuu wa ubakaji' New Delhi, polisi wameweka bayana takwimu kwamba kesi nyingi takribani 706 za ubakaji - karibu mbili kwa siku - zimefunguliwa mwaka 2012, ambazo ni takribani asilimia 24 zaidi ya kesi 572 zilizoripotiwa mwaka 2011.

No comments: