Hili ndilo gari walilokuwa wakisafiria walimu hao watano ambao walipoteza maisha. |
Miili ya walimu watano wa Shule ya Sekondari Scolastika ya Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, waliokufa ajalini wakitoka katika msiba wa mwanafunzi wao mkoani Arusha, itaagwa leo kuanzia saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Manispaa ya Moshi.
Akizungumza jana, Mkuu wa Shule hiyo, Scolastica Shayo, alisema watu watapata fursa ya kuiaga miili hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda katika nchi wanazotokea, ambazo ni Kenya na Uganda.
Shayo alisema baada ya kumaliza kuaga miili hiyo, itasafirishwa leo kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi, ambapo alieleza kuwa ndugu wa marehemu wanaotokea Kenya na Uganda, tayari wameshafika nchini kwa ajili ya kusafirisha miili ya ndugu zao.
Akizungumzia majeruhi wanne ambao ni walimu wa shule hiyo, Shayo alisema hali zao zinaendelea vizuri, isipokuwa dereva aliyekuwa akiwaendesha walimu hao ameonekana kuumia vibaya zaidi.
Ajali hiyo ilitokea Desemba 10, mwaka huu saa 2:30 katika kona ya mto Kikavu wilayani Hai baada ya gari walilokuwa wakisafiria, Toyota Hiace lenye namba za usajili T771 AQD, kugongana na Scania, mali ya Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers, yenye namba za usajili T212 AHH, yenye tela namba T653 AAJ, likitokea Moshi kwenda Kwasadala.
Katika ajali hiyo iliyoleta simanzi kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na uongozi wa wanafunzi wa Scolastica, walimu watano waliokufa, watatu ni Wakenya, Mganda na Mtanzania.
Waliofariki ni Julius Kimaro mkazi wa Rombo mkoani Kilimanjaro, Bernard Omukunyu, Erinst Ambani na Nelly Sasaka ambao ni Wakenya na Joseph Opolochi ambaye ni Mganda.
Waliojeruhiwa wengine ni pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Shule hiyo, Peter Mlai, Dismas, Nelson wote wakiwa ni walimu na Alexander Mocha, ambaye ni dereva wa gari la shule hiyo.

No comments:
Post a Comment