MILIONEA MVUMBUZI WA "MCAFEE ANTIVIRUS" AACHIWA HURU GUATEMALA...

John McAfee.
John McAfee, milionea ambaye amevumbua na kutengeneza programu ya kuzuia virusi vya kompyuta ya McAfee 'McAfee Antivirus' ameachiliwa kutoka rumande nchini Guatemala, ambako alikamatwa kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume cha sheria, huku akiendelea kuchukuliwa kama 'mtu muhimu' katika kesi ya mauaji ya mkazi wa Belize.
Baada ya kuachiwa kwake, McAfee mwenye miaka 67 aliwaambia waandishi wa habari, "Niko huru. Ninakwenda Marekani." Alisema anapanga kupanda ndege kuelekea Miami.
Maofisa Uhamiaji wa Guatemala tayari wamemsindikiza McAfee hadi Uwanja wa Ndege wa jiji la Guatemala.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, McAfee amekuwa akikimbia kimbia tangu alipotajwa mtu muhimu katika mauaji ya jirani yake huko Belize -- ambako McAfee amekuwa akiishi kwa miaka kadhaa.
Wanasheria wa McAfee wamesema kumrejesha gwiji huyo wa programu Belize kunaweza kufuatiwa na hukumu ya kifo ... sababu McAfee "amezishutumu mamlaka."

No comments: