![]() |
| Abiria wakipanda treni tayari kuanza safari kwenye stesheni ya Dar es Salaam. |
Usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Mwanza uliokuwa umesimama tangu mwaka 2009, hatimaye umerejeshwa rasmi.
Jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe alizindua kuanza kwa safari hiyo jana mnamo saa 8:30 mchana katika Stesheni Kuu ya reli hiyo, Dar es Salaam.
Mara baada ya kuzindua safari hiyo kwa kuipungia bendera maalumu ya kijani kama ishara kwa dereva kuanza safari, Dk, Mwakyembe aliushuruku uongozi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL) kwa kujituma bila ya kujadili maslahi duni waliyonayo.
Aidha aliahidi kuwa kilio chao kitazingatiwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa morali yao inazidi kuimarika kwa lengo la kukabili changamoto ya azma ya Serikali unaotokana na uamuzi wake wa kuwekeza katika uimarishaji wa miundo mbinu ya reli na ununuzi wa vitendea kazi vipya na hivyo kurejesha huduma za reli katika kiwango chake cha kawaida ili kukidhi mahitaji ya wateja wa ndani na wa nje.
Katika safari ya jana, takribani abiria 1,000 waliondoka, wakiwemo wa kuelekea mikoa ya Dodoma, Tabora, Kigoma, Mpanda na Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu, safari za treni hiyo zitakuwa zinafanyika kila siku za Jumanne na Ijumaa.
Wakati wa uzinduzi huo, Dk,. Mwakyembe alifuatana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Uchukuzi akiwemo Katibu Mkuu, Mhandisi Omar Chambo. Treni hiyo inatarajiwa kupokewa asubuhi ya leo jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba.
Huduma ya usafiri wa treni ya abiria kwenda Mwanza ulisitishwa mwishoni mwa mwaka 2009 kutokana na ukosefu mkubwa wa vichwa vya treni na mabehewa ya abiria.
Hata hivyo mara baada ya safu za Uongozi wa Dk Mwakyembe na Naibu wake Dk Tizeba kuteuliwa kuongoza Wizara ya Uchukuzi Mei mwaka huu waliweka juhudi kuona rasilimali zinapatikana kuwezesha huduma ya treni inaimarika ikiwemo kwanza huduma ya treni ya Jiji la Dar es Salaam na pia ya kwenda Mwanza.

No comments:
Post a Comment