![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah. |
Wadau katika mapambano dhidi ya rushwa wameibana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wengi wakielezea kutoridhishwa na utendaji wao kazi katika masuala mbalimbali yanayohusiana na rushwa, huku wakitaka sheria ya rushwa itumike ipasavyo.
Hatua hiyo, imekuja kutokana na maelezo kwamba, taasisi hiyo imekuwa ikijivuta mno katika kufuatilia taarifa au kesi mbalimbali za rushwa, nyingine zikiwa za wazi na ambazo watu hujitokeza hadharani wakidai wana ushahidi wa vitendo hivyo.
Wadau hao walitoa maoni yao jana jijini Dar es Salaam wakati wa mdahalo ulioandaliwa na Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Sekretarieti ya Maadili ya Umma na Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa yatakayoadhimishwa nchini keshokutwa Jumatatu.
Mmoja wa wadau hao, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alibainisha wazi kuwa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye alitakiwa kuitwa Takukuru kusaidia katika kukamata watoa rushwa baada ya kuzungumza na waandishi kuwaambia kuwa aliangushwa na mtandao wa Rushwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM wilayani Hanang.
Katika uchaguzi huo, Sumaye alijitoksa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia wilaya ya Hanang, akichuana na Dk. Mary Nagu, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang. Dk. Nagu aliibuka mshindi.
Akirejea `kilio’ cha Sumaye, Lipumba alisema kwa kutomuita Sumaye na kuwakamata watoa rushwa katika mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM imeonesha wazi udhaifu wa taasisi hiyo, kwani inaaminika asilimia 70 ya waliochaguliwa wametokana na rushwa.
“Katika chama kilichoshika dola kumekuwa na malalamiko mengi ya mtandao wa fedha kuweka watu wao katika chama jambo ambalo ni mtandao kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015 sasa kwa nini watu hao hawajaitwa kusaidia kubaini watoa rushwa kwa manufaa ya baadaye?,” alihoji Profesa Lipumba.
Aliongeza kuwa, yapo masuala mengi ambayo taasisi hiyo wamekuwa wakiyafumbia macho, akitolea mfano suala la watu waliorudisha fedha za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na nyinginezo.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Jaji Kiongozi (Mstaafu) Ramadhan Manento alisema ana wasiwasi Takukuru na utendaji wa Takukuru, akisema kuna waliokamatwa kwa rushwa na kesi zao kufikishwa mahakamani, lakini kesi haziendi.
Alitolea mfano kuwa, kuwa WanaCCM waliodaiwa kukamatwa kwa rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi mwaka 2010 na kesi zao kufikishwa mahakamani, lakini kesi zao zinasuasua.
Aidha, Jaji Manento alisema viongozi wengi wa Serikali wamekuwa wakituhumiwa na masuala mbalimbali lakini mara zote Takukuru imekuwa ikitaka wenye ushahidi wajitokeze, jambo alilosema linashangaza hasa ikizingatiwa chombo hicho kina nguvu kisheria ya kupenya kokote, hata serikalini ambako chenyewe ni chombo cha Serikali.
Jaji alitaka kufuatwa kwa sheria na kuacha kutumia maneno ya wanasiasa kuacha kuweka vya kwao ikiwa ni pamoja na kutumia utawala bora kwa kufuata sheria za kiserikali.
Naye James Marenga wa Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria (NOLA) alisema mapambano ya rushwa kwa sasa yamekuwa yakifanywa kwa chuki na kukomoana kwani kuna kesi nyingi hufikishwa mahakamani bila ushahidi wa kutosha na hivyo kuigharimu serikali fedha nyingi.
Alisema ili kupambana na rushwa, Takukuru inapaswa kuacha `siasa’ ndani ya mapambano ya rushwa ili matokeo yapimwe kwa jinsi inavyopambana, na si maneno mengi.
Naye Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema hata kukiwa na vyombo vingi kama Takukuru, watu wanaweza kujificha na kuendelea na vitendo vya rushwa, huku akishauri dawa pekee ni kwa watu kuwa na hofu ya Mungu kwani mbele ya Mungu haiwezekani mtu kula rushwa na bado akaweza kujificha.
Akiwasiisha mada yake katika mdahalo huo, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo alisema changamoto kubwa Iliyopo katika mapambao na Rushwa ni pamoja na ushirikiano duni kati ya Serikali na Sekta binafsi pamoja na umakini wa watendaji serikalini kupambana na rushwa.
Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni kuchukua muda mrefu katika kuthibitisha makosa ya rushwa, jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi na kutumia muda mfupi kushughulikia vitendo hivyo ili viishe.
Pia alisema mbali na changamoto hizo, lakini hadhi ya Taznzania katika mapambano dhidi ya Rushwa imeendelea kuboreshwa kwa viwango vya kmataifa kuanzia mwaka 2004 kiwango cha alama kimefikia alama tatu mwaka 2010.
Mwasilisha mada mwingine, Ayoub Ryoba ambaye ni mwanahabari mkongwe na mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) alisema vyama vya siasa vionyeshe utashi katika kupinga rushwa kuanzia safu zake za uongozi na katika michakato ya uchaguzi ndani ya vyama.
Alisema pia,viongozi wa juu kitaifa waonyeshe mfano wa uadilifu kwa vitendo huku taasisi zinazosimamia mapambano dhidi ya rushwa zikipaswa kushirikiana kimkakati.
Mtoa mada mwingine kutoka Taasisi ya Vijana, Gwakisa Makaranga aliwataka vijana kuwajibika na kuacha dhana kuwa yeyote aliyepata utajiri ni fisadi huku akiwasihi kuacha kutumia muda mwingi kwa anasa. Aidha, amewasihi wanasiasa kuwatumia vijana kwa kuwajengea mwenendo mzuri na siyo kuwatumia kwa kuwapa rushwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Kimataifa (UNDP), Alberic Kacou, alisifia Tanzana kwa juhudi za kupambana na rushwa akiitaja kuwa ni ya tatu kwa mapambano miongoni mwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha alisema mdahalo huo ni sehemu ya maadhimisho yenye Kaulimbiu ya ‘Chukua Hatua dhidi ya Rushwa Sasa’ inayoadhmishwa Desemba 9 kila mwaka lakini kwa Tanzania, itaadhimishwa Desemba 10 ili kupisha sherehe za Miaka 51 ya Uhuru.
Alisema katika kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma kuhusiana na uadilifu,uzalendo na utawala bora wamejadiliana ili kuainisha mitaala ya elimu kuhusiana na masuala hayo kuanzia shule ya msingi,Sekondari na vyuo.
“Tunaendelea na mchakato wa kuweka kwenye mitaala kwa shule za msingi tumeishajadiliana na wadau wakuu wa elimu wizarani na kwenye taasisi za elimu kama vyuo vikuu tumekutana na wadau, kwa sasa uchambuzi wa mada unaendelea,” alisema.
Alisisitiza kabla ya hatua hiyo, kwa sasa wameanzisha klabu 400 katika shule za Sekondari zenye wanachama zaidi ya 2,700 wanaopata uelewa wa kina juu ya masuala ya rushwa na athari zake.

No comments:
Post a Comment