Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. |
Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,814 wakiwemo wenye magonjwa yasiopona na wajawazito katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika jana nchini.
Mbali na kutoa msamaha huo, Rais Kikwete ambaye jana aliongoza sherehe za maadhimisho hayo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, amewataka Watanzania kuendeleza amani, umoja na mshikamano.
Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu wafungwa wenye makosa ya ubakaji, ulawiti, kuwapa wanafunzi mimba, waliotumia madaraka vibaya na wala rushwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ilieleza kuwa, Rais Kikwete ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wafungwa walionufaika na msamaha huo kutokana na ugonjwa ni waliothibitika kuwa na Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na saratani ambao wako katika hali mbaya. Mbali na wagonjwa, wapo pia wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.
“Wamo waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kuwepo gerezani kwa ridhaa ya Rais wa Tanzania chini ya kifungu cha 26 cha Kanuni ya Adhabu, ambao hadi Desemba 9, mwaka huu wamekaa gerezani si chini ya miaka mitano na wamekuwa na tabia njema,” alisema Dk Nchimbi akifafanua zaidi kuliko wanufaika hao.
Wengine ni wafungwa wanawake walioingia na mimba au na watoto wadogo gerezani, wenye ulemavu wa mwili na akili, wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na walikwishatumikia robo ya kifungo chao.
Dk Nchimbi alisema kutokana na madaraka hayo, Rais Kikwete ametoa msamaha huo kwa wafungwa 3,814 na wafungwa wenye matatizo maalumu kati ya waliosamehewa, wamethibitishwa na jopo la madaktari chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Wilaya husika.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msamaha huo hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, kifungo cha maisha, waliofungwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, waliotoa au kupokea rushwa na wenye makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa magari kwa silaha.
Pia hauwahusu waliopatikana na makosa ya kunajisi, kubaka na kulawiti, waliowapa wanafunzi mimba, walioharibu miundombinu kama kuiba nyaya za simu, umeme au mafuta ya transfoma na waliokutwa na silaha au risasi.
Dk Nchimbi alisema wengine wasiohusika ni wafungwa wazoefu wanaotumikia kifungo cha pili na kuendelea, waliowahi kupewa msamaha lakini wanatumikia sehemu ya kifungo kilichobaki, waliowahi au kujaribu kutoroka na waliotumia madaraka vibaya.
Wengine ni waliohukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kusoma na wale wanaotumikia kifungo chini ya Sheria namba 25 ya mwaka 1994 ya Bodi ya Parole na Sheria ya Huduma kwa Jamii Namba 6 ya mwaka 2002.
Katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka jana, Rais Kikwete alitoa msamaha kwa wafungwa 3,803 na mwaka 2010 katika shehere kama hizi alisamehe wafungwa 3,563.

No comments:
Post a Comment