CHEKA TARATIBU...

Mzee mmoja wa Kinyakyusa katika miaka ya 1990 kaja Dar kwa lengo la kumtafuta mwanawe aliyezamia jijini humu kwa miaka mingi bila mawasiliano. Moja kwa moja basi alilopanda likamshushia maeneo ya Kariakoo. Kwa takribani saa nzima aliyokuwa akizunguka alikuwa akiona maghorofa yaliyoandikwa "Msajili wa Majumba". Mwishowe yule mzee akapiga kelele kwa sauti, "Mwee, Mweeee. Yani mimi ninavyoteseka kule kijijini kumbe mwanangu ASAJILE MWAIJUMBA anamiliki maghorofa kibao huku mjini!" Kasheshe...

No comments: