![]() |
| KUSHOTO: Mchoro wa tattoo katika mkono wake wa kushoto. KULIA: Mhusika mwenyewe. |
Wapelelezi wametoa hadharani picha ya mwanaume ambaye wanakusudia kumfanyia uchunguzi baada ya mwili wake kuanguka kutoka sehemu ya chini ya ndege iliyokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow.
Polisi waliitwa eneo la Portman Avenue, Mortlake, ambayo iko kwenye ukingo wa kusini wa Thames, Saa 2 asubuhi ya Jumapili Septemba 9, kufuatia taarifa kwamba kuna mwili umedondoka kutoka angani.
Mwanaume huyo hakuwahi kutambuliwa, lakini anaaminika kuwa ni Mwafrika mwenye umri wa kati ya miaka 20 na 30.
Jana polisi walisambaza picha mbili za mwanaume, baada ya 'juhudi za matangazo ya awali' kushindwa kumtambua mtu huyo.
Inadhaniwa kwamba mwili wa mtu huyo ulidondoka kutoka kwenye ndege chini ya sehemu ya gurudumu wakati ndege hiyo ikijiandaa kutua.
Wataalamu wa usafiri wa anga wamesema mtu huyo inawezekana alishakufa kabla hajatua ardhini pengine sababu alikuwa amegongwa na gudurumu muda baada ya ndege hiyo kuruka, au sababu ya baridi kali katika eneo la juu kutoka usawa wa bahari.
Mtu huyo, ambaye alikuwa na urefu wa futi 5 na inchi 4 na mwili uliojengeka kiasi, hakuwa mmoja wa abiria au wafanyakazi wa ndege hiyo.
Wakati huo, wakazi wa barabara tatu huko Mortlake, ambako ni umbali usiozidi maili kumi kutoka uwanja wa ndege, wameeleza mshituko wao kugundua mwili huo baada ya kusikia kishindo kikubwa.
Mmoja alisema: "Huwezi kuamini. Kitu cha kwanza nilichofikiri nilipoona mwili huo ilikuwa kwamba lazima utakuwa umeanguka kutoka umbali mrefu juu."
Uchunguzi ulifanyika katika Hospitali ya Kingston Mortuary Septemba 11 na kutaja sababu za kifo kuwa ni majeraha kadhaa.
Msemaji wa polisi alisema: "Inawezekana alikuwa akitokea Angola kufuatia kukutwa na fedha za Angola katika mifuko yake na taarifa zimebainisha kuwa ndege kutoka Luanda, Angola ilikuwa imewasili muda mfupi baada ya mwili huo kugundulika."
Mwanaume huyo alikuwa kavalia jeans, fulana ya kijivu na raba nyeupe wakati alipodondoka, na kwamba alikuwa na mchoro wa tattoo katika mkono wake wa kushoto yenye alama ya herufi za 'Z' na 'G' zinazoonekana wazi.
Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga alisema mzamiaji anayejificha kwenye magurudumu ndege hana nafari ya kupona kutokana na pengine kugongwa na magurudumu baada ya kuruka ay kuganda kwenye nyuzijoto chini ya -40C (-40F).
Alisema: "Nafasi ya kunusurika kifo kwa mzamiaji ni finyu mno, hasa kwenye sehemu ya magurudumu.
"Sina taarifa zozote za mtu aliyewahi kuzamia na kupona katika ndege za masafa marefu.
"Wakati magurudumu yanapochomoza chini upande mwingine, maili chache kutoka barabara ya kurukia ndege na takribani futi 2,000 angani, kama kuna mtu aliyekufa lazima ataanguka nje."
Ugunduzi huo umekuja siku kadhaa baada ya mwili wa mzamiaji kukutwa kwenye magurudumu muda mfupi baada ya ndege ya British Airways kuwasili Uwanja wa Ndege wa Heathrow ikitokea Cape Town, Afrika Kusini.

No comments:
Post a Comment