Mume wakati akitoka kazini mara kwa mbali akamwona mkewe akija huku kashikana mikono na jamaa mwingine. Mume ili afumanie vizuri akaamua kupanda juu ya mti wa jirani. Mkewe na yule jamaa yake bila kujua wakaja na kusimama kivulini chini ya ule mti. Haukupita muda yule jamaa akaanza kumwaga sera zake na kumalizia hivi, "Yani ninavyokupenda ajuaye ni aliye juu!" Mume kule juu akajibu kwa ukali, "Mimi sijui chochote!" Balaa...

No comments:
Post a Comment