Sunday, December 9, 2012

HII NDIO AJALI ILIYOUA WATANO WA FAMILIA MOJA...

Hili ndilo gari aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BNP lililopata ajali majira ya 6:30 mchana eneo la Tanangozi, mkoani Iringa Jumanne iliyopita. Gari hili lilikuwa likiendeshwa na Ezekiel Mwaiteleke (marehemu) na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo. Tunawasihi madereva wote kuwa makini barabarani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya ambapo rekodi zimeonesha ongezeko kubwa la ajali katika miaka ya hivi karibuni.

No comments: