Kamanda Robert Boaz. |
Polisi mkoani Kilimanjaro inamsaka Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tarakea iliyopo Wilaya ya Rombo, Samson Lyimo (27) kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza (jina limehifadhiwa).
Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa mwalimu huyo ana rekodi ya matukio ya ubakaji.
Alitoa mfano kuwa, mwalimu huyo akiwa anafundisha katika Shule ya Sekondari Makiidi alimpa ujauzito mwanafunzi wa shule hiyo, na baadaye kuhamia katika Shule ya Sekondari Nanjararera alikoonekana kuwa na tabia chafu kabla ya kuondoka na kuhamia Shule ya Sekondari ya Tarakea.
Kamanda Boaz alisema Jeshi la Polisi limeanza msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ambaye alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na kutokomea kusikojulikana.
Awali ilidaiwa kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15, alibakwa na mwalimu wake huyo, baada ya kumfungia nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Tarakea, Maritine Kija, mwanafunzi huyo alibakwa Novemba 30, mwaka huu na mwalimu huyo baada ya kumtuma dukani nje kidogo ya shule kukunua gundi aina ya super glue.
Kija alibainisha kuwa baada ya mwanafunzi huyo kununua gundi hiyo alimpelekea mwalimu huyo ambaye alimwagiza aipeleke nyumbani anapoishi, ambapo baada ya kufika alimkuta kijana wa kiume (jina halikufahamika) ambaye badala ya kuipokea alimwagiza aipeleke chumbani mwenyewe.
Alisema baada ya mwanafunzi huyo kuingia ndani ya chumba cha mwalimu huyo kwa lengo la kuweka gundi hiyo, mara alitokea mwalimu huyo na kuingia ndani kisha akafunga mlango na kuanza kumbaka.
Kija alisema baada ya mwalimu huyo kukidhi haja yake, mwanafunzi huyo alitoka ndani huku akilia na kwenda kuripoti kwa Mkuu wa Shule, na baadaye uongozi wa shule ulitoa taarifa Polisi.
Alisema mwanafunzi huyo alipelekwa katika Kituo cha Afya Tarakea kwa ajili ya matibabu ambako pia vipimo vilionesha kuwa alibakwa.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa shule alibainisha kuwa mwalimu huyo hakuwa mwajiriwa shuleni hapo bali alikuwa akifundisha kwa mkataba, ambao ulianza Novemba mosi mwaka huu na ulitarajiwa kumalizika Januari 31, mwakani.
Kwa upande wa baba wa mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina moja la Paulo, alikiri mtoto wake kubakwa na kueleza kuwa alichaniwa nguo zake za ndani pamoja na kutokwa na damu nyingi sehemu za siri, na kwamba hospitali alipatiwa dawa ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi.
Aliliomba Jeshi la Polisi kutumia taaluma yake kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe kwenye mikono ya sheria.

No comments:
Post a Comment