MASHAHIDI WA KESI ZA PEMBEJEO WAFICHWA ZAMBIA...
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rukwa (Takukuru) mkoani Rukwa imekiri kuwa baadhi ya mashahidi muhimu katika kesi ya wizi wa mbolea katika mfumo wa vocha zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200 wamekimbilia nchi jirani ya Zambia, baada ya kuhongwa na baadhi ya watuhumiwa ili wasitoe ushahidi mahakamani dhidi yao.
Hayo yalibainishwa jana na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Rukwa, Gasto Mkono alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambao walitaka kujua kwanini kesi hizo zimechukua muda mrefu huku Takukuru ikishutumiwa na jamii kuwa imehusika kuvuruga ushahidi wa kesi hizo .
Alisema kuwa kushindwa kupatikana kwa mashahidi hao muhimu katika kesi hizo kumekuwa kikwazo kikubwa katika mwenendo mzima wa mashauri hayo mahakamani.
Akifafanua alidai kuwa zaidi ya majalada 40 yamepelekwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) ambapo majalada 18 yamerudi na yapo mahakamani, lakini tatizo kubwa mashahidi hawapo tena tayari kutoa ushahidi wao mahakamani kwa kuwa baadhi ya washitakiwa wengi wao wakiwa ni mawakala ‘wamewahonga’ mashahidi hao ambao baadhi yao wamekimbilia nchi jirani ya Zambia ili wasiweze kutoa ushahidi.
“Tunafanya kazi katika mazingira magumu, mahakamani kuna majalada 18 ya kesi ya watuhumiwa wa mbolea kwa mfumo wa vocha, baadhi yao sasa wanamiliki magari ya kifahari na hata nyumba lakini tatizo wanaotakiwa kutoa ushahidi hawako tayari kufanya hivi tena.
“Wapo mashahidi muhimu wanaotakiwa kutoa ushahidi wao mahakamani, lakini kila tukiwafuata wanakimbilia Zambia na kujificha hadi hapo watakaposikia kuwa tumerejea tulikotoka…
“Hii inatoka na baadhi ya watuhumiwa kuwahonga mashahidi hao muhimu. Sasa hata kama tulikusanya ushahidi wa kutosha sasa tumekwama kwa kuwa mashahidi hawako tayari tena kutoa ushahidi mahakamani,“ alisema .
Aliongeza kuwa baadhi ya maofisa watendaji wa vijiji wakati Takukuru ilipokuwa ikikusanya ushahidi walikiri hawakufikishiwa mbolea za ruzuku kwa mfumo wa vocha, lakini baadaye walipotakiwa kutoa ushahidi mahakamani “waliwavua’ tuhuma hizo washtakiwa kwa kukiri walipokea mbolea hizo kutoka kwa washitakiwa.
“Hii maana yake ni kwamba mawakala ambao baadhi yao ni watuhumiwa wanadaiwa kuwahonga maofisa hao watendaji wa vijiji ili wasitoe ushahidi dhidi yao hivyo kutokuwepo ushahidi wa kuwatia hatiani,“ alisema .
Kuhusu Takukuru na shutuma za kuvuruga ushahidi, Kamanda Mkono alikana shutuma hizo kwa kuwa ni mashahidi wenyewe ambao sasa hawako tayari tena kutoa ushahidi mahakamani lakini pia ililazimu Takukuru kufanya uchunguzi wa kina na kukusanya vielelezo vingi kisha kuyatuma majalada zaidi ya 40 kwa DPP ambapo tayari 18 yamesharejeshwa.
Alisema kuwa majalada 40 yalifikikwa kwa DPP kufuatia tuhuma za ‘uchakachuaji‘ wa mbolea ya ruzuku katika mfumo wa vocha zilizobainika kufujwa na baadhi ya mawakala wakishirikiana na watendaji wa vijiji ambapo ilimlazimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa wakati huo, Daniel ole Njoolay kuunda kamati ya kuchunguza tuhuma hizo uliofanyika katika msimu wa kilimo wa 2008/09 .
Kamati hiyo katika uchunguzi wake ilibainisha kuwa zaidi ya mbolea za ruzuku katika mfumo wa vocha zenye thamani ya Sh bilioni 5 zilikuwa zimefujwa .
Hata hivyo, Kamanda Mkono alidai kuwa Kamati hiyo iliyoundwa Njoolay ilikuwa ya kisiasa kwa maana kwamba haikuwa na mamlaka kisheria kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, ndiyo maana Takukuru ililazimika kufanya tena uchunguzi wa kina na kukusanya vielelezo na ushahidi wa kutosha dhidi ya watuhumiwa.
Pia alikiri kuwa Takukuru imeshindwa katika kesi nyingi walizozifikisha mahakamani si kwa kuwa hawakuwa na ushahidi, bali changamoto kubwa ni upande wa jamii yenye kusita kutoa ushahidi mahakamani.
Comments
Take a look at my web page - review of google sniper
know-how, therefore it's good to read this blog, and I used to visit this weblog every day.
My web blog Http://chestfatburner.com/how-can-i-diagnose-gynecomastia-at-home/
You understand therefore considerably relating to this matter, produced
me individually imagine it from a lot of various angles.
Its like men and women aren't involved unless it is one thing to do with Girl gaga! Your personal stuffs great. All the time maintain it up!
Here is my page; Saggy Torso And Also Gynecomastia
think. Also, many thanks for allowing for me to comment!
Here is my web-site - Several concealed information about " moobs "
Also visit my blog - chest muscle tissue and also the minimize period
When I look at your blog in Safari, it looks fine however, when opening in Internet Explorer, it's got some overlapping issues. I just wanted to give you a quick heads up! Apart from that, wonderful blog!
Feel free to visit my homepage - Loose people unpleasant moobs
against hackers? I'm kinda paranoid about losing everything I've worked hard on.
Any tips?
my weblog :: Is actually gynecomastiarelated with anabolic steroid drugs?
Does one offer guest writers to write content for you personally?
I wouldn't mind composing a post or elaborating on a lot of the subjects you write about here. Again, awesome weblog!
my site :: Meals reponsible with regard to development of man boobs
weblog on regular basis to taаke upԁated from neԝest newѕ.
Several of them are rife with spelling problems and I find it very troublesome to inform thhe reality however I'll ceгtainly come
back again.