WATHIBITISHA USEMI WA WAHENGA "KUFA KUFAANA"

Watu wasiofahamika wakisomba nyanya zilizosambaa barabarani baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Sangasanga, Kata ya Mzumbe, wilayani Mvomero, Barabara Kuu ya Iringa – Morogoro, usiku wa Alhamisi iliyopita. Ajali hiyo ilisababishwa na lori aina ya Mitsubishi Fuso iliyobeba matenga ya nyanya kutoka Iringa kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake ndipo lilipokutana na gari jingine lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Iringa na katika harakati za kulikwepa likajibamiza kwenye lori kubwa lililokuwa upande mwingine na kupinduka. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, inadaiwa mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.


No comments: