WATOTO WA MIAKA MITATU WAWACHENGUA MARAIS SHEREHE ZA UHURU...

Watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu kila mmoja wakishiriki kikamilifu katika kucheza na kupiga ngoma sambamba na wasanii wengine wa kikundi cha ngoma cha Utandawazi kutoka Ukerewe, mkoani Mwanza mapema leo katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo marais kadhaa wa nchi za Afrika walihudhuria. Watoto hao walikuwa kivutio kikubwa kutokana na ustadi wao katika kufuatisha midundo kiasi cha kuwafanya baadhi ya waalikwa kwenda kuwatuza fedha.

No comments: