Kijana wa miaka 20, Adam Lanza amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga risasi. Baada ya hapo alienda katika shule ya msingi na kuua watu wengine 30, wakiwemo wanafunzi 20 – wa umri wa kati ya miaka mitano na 10.
Mauaji hayo ya kusikitisha, yalifanyika juzi katika Shule ya Msingi ya Sandy Hook Jimbo la Connecticut nchini Marekani.
Ofisa wa Polisi katika jimbo hilo, Paul Vance alisema walipata habari ya tukio hilo saa tatu na nusu asubuhi. Walipofika katika shule hiyo, walikuta miili mingi, ikiwemo ya wanafunzi, walimu na mwili wa mshambuliaji huyo.
Vance alisema idadi halisi ya waliokufa, itatangazwa baada ya kuwaarifu ndugu na jamaa za watu waliouawa.
Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo ni Mkuu wa Shule hiyo, Dawn Hochsprung ambaye amekuwa katika uongozi wa shule hiyo tangu 2010.
Hivi karibuni Hochsprung aliweka picha akiwa kazini kwake katika mtandao wake wa tweeter na alielezea kinachoendelea shuleni kwake.
Siku nne kabla ya kifo chake, aliweka picha za watoto wawili wa chekechea, wakinunua bidhaa katika mashine ya kulipia ya kutengenezesha iliyokuwa darasani, akielezea kitendo hicho kama njia ya kufundisha watoto masuala mbalimbali ya kimaisha.
Akizungumza baada ya mauaji hayo, Rais Barack Obama aliyeonekana kujawa na huzuni na mara kadhaa akifuta machozi, alitoa mwito wa kutaka zichukuliwe hatua za kuzuia mauaji ya kutumia bunduki.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema walisikia milio mia moja ya risasi na kuwaona watoto waliokuwa wakihofia maisha yao, wakilikimbia jengo la shule hiyo.
Rais Obama ameamuru bendera ya Marekani, ipepee nusu mlingoti kwenye majengo ya Taifa.
Akizungumza juu ya mauaji hayo, Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard alisema tukio hilo linasikitisha zaidi, kwa vile waliouawa ni watoto.

No comments:
Post a Comment