Sunday, November 18, 2012

WAZIRI WA ZAMANI JACKSON MAKWETTA AFARIKI DUNIA...

Waziri wa zamani Jackson Makwetta amefariki dunia jana Saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.
Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye.
Bw. Makwetta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.
Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.

No comments: