| Kamanda Anthony Rutta. |
Polisi mkoani Tabora inamsaka mume wa Katarine Lubinzo, Liana Masesa (56) mkazi wa Kijiji cha Loya Wilaya ya Uyui kwa tuhuma za kumpiga na mchi mkewe kichwani na kumuua.
Tukio hilo lilitokea Novemba 14, mwaka huu katika kijiji cha Loya Wilaya ya Uyui majira ya saa 2 usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Anthony Ruta alisema kwa mujibu wa maelezo ya walioshuhudia, mtuhumiwa alimuua mkewe baada ya kuzuka mtafaruku kuhusu lilipo dumu la maji.
Ruta alisema mara baada ya kufanya mauaji hayo, mtuhumiwa alitoroka na Polisi wanaendelea kumsaka.
Alisema ugomvi uliosababisha kifo cha mama huyo ungeweza kuepukika kama mtuhumiwa angemsikiliza mke wake, kwani inasemekana dumu hilo lilikuwa limehifadhiwa nyumba ya pili.

No comments:
Post a Comment