Tuesday, November 20, 2012

WANAJESHI WALIOMUUA SWETU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KIFO...



Wanajeshi waliohukumiwa kifo, Koplo Ally Ngumbe (kushoto) na Sajenti Roda Robert. Picha ndogo ni Marehemu Swetu Fundikira.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam muda mfupi uliopita imewahukumu adhabu ya kifo wanajeshi watatu waliohusika kumpiga na kumsababishia kifo Swetu Fundikira baada ya kupatikana na hatia. 
Wanajeshi hao ni MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi. Mwanajeshi wa tatu alitoroka mara baada ya tukio.
Swetu alifariki Jumapili asubuhi ya Januari 25, 2010 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa kwa siku mbili baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa wanajeshi hao watatu, ambapo wawili walifanikiwa kukamatwa na mwingine kutokomea kusikojulikana huku msako mkali ukiwa bado unaendelea.
Kifo hicho kilizua mtafaruku mkubwa miongoni wa wananchi ambao walikemea vikali tabia ya askari kupiga raia na kuutaka viongozi wa jeshi kuwa wakali katika kuwadhibiti askari wachache wanaotumia vibaya madaraka yao.
Marehemu Swetu alizikwa katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

No comments: