![]() |
| Abdulrahman Kinana. |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameagiza kuanzia sasa wanachama wa chama hicho nchini kuacha kuitana waheshimiwa badala yake waitane ndugu kama alivyopendelea Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Kinana alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na viongozi wa CCM, mjini hapa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne ya kujitambulisha na kukagua uhai wa chama hicho mkoani hapa na mikoa ya Mtwara, Geita na Arusha.
"Mimi katika maisha yangu ya kumfahamu Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere, sikupata kumsikia akijiita au akitaka aitwe Mheshimiwa Mwenyekiti au Mheshimiwa Rais, sasa haya mambo ya sisi kuitana mheshimiwa tunayatoa wapi?" Alihoji Kinana.
Alisema Mwalimu Nyerere hakujiita mheshimiwa kwa sababu ina maana kubwa sana, kwa hiyo ni lazima wana-CCM kuendeleza utamaduni huo wa kuitana ndugu kwa sababu unazuia matabaka.
Kuhusu makundi ndani ya CCM, Kinana alisema chama hicho kitamtosa bila kumwonea haya mwanachama atakayeomba kuteuliwa kugombea urais huku akiwa kinara wa kutegemea makundi kumwingiza kwenye nafasi hiyo.
Badala yake CCM itahakikisha mgombea inayemsimamisha ni mwana CCM asiyeendekeza makundi, mwadilifu ambaye kila akiteuliwa atakuwa hatiliwi shaka.
Kauli hiyo ilitokana na swali la mwanachama Peter Lilata akitaka kujua CCM imejiandaa vipi kuhakikisha katika uchaguzi mkuu wa 2015, inateua mgombea atakayekubalika na wananchi wengi, na kutofanya kosa kuteua mgombea asiyekubalika kwani kufanya hivyo kutaisababishia usumbufu mkubwa katika kupata ushindi.
Akizungumzia rushwa na mizengwe katika uchaguzi, Kinana alitaka wana CCM kuhakikisha katika kila uchaguzi waunge mkono wagombea watendaji wazuri na wenye maadili safi badala ya kukumbatia wanaowapa rushwa.
"Lazima mjue kwamba, mnapoamua kumchagua mgombea anayewapa rushwa, mnafanya kosa kubwa sana kwenu, maana akishapita anakuwa kiongozi wa kutetea maslahi yake na si yenu," alisema Kinana.
Alisema, pamoja na kuwapo viongozi wanaotoa rushwa kutafuta uongozi, lakini, wananchi nao wamekuwa chanzo cha kukomaza rushwa kwa sababu mwanachama mwenzao anapojitokeza kuomba uongozi, huwa wa kwanza 'kutengeneza' mazingira ya kumtaka atoe rushwa huku wakionesha kwamba hawezi kupenya bila hivyo.
Kuhusu utayari wake, Kinana aliwahakikishia Watanzania, hususan wana CCM kwamba yuko tayari kimwili na kiakili kutekeleza kwa ufanisi mkubwa majukumu aliyopewa kulitumikia Taifa.
"Ni kweli nilikuwa nimetangaza kustaafu siasa, kwa kuzingatia kwamba nimeshashika kwa muda mrefu nyadhifa za kuchaguliwa, nikaona kama wenzako wameshakwamini kwa muda mrefu ukafanya nao kazi wakikupenda, basi usisubiri uchokwe ndipo uondoke.
"Lakini baada ya uamuzi wangu, Mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete akaamua kwa kadri alivyoona inafaa, kuniteua nikisaidie chama. Kwa mtu mwenye hekima na uadilifu, unapoteuliwa na Mwenyekiti wa Chama chako, tena Rais, lazima ukubali tena bila kinyongo, nikakubali."
Aliongeza: "Sasa baada ya kuwa mimi ndiye Katibu Mkuu wa Chama hiki, napenda kuwaambia kwa dhati ya moyo wangu, kwamba nipo tayari kimwili na kiakili kuhakikisha nawatumikia wana CCM na Watanzania kwa jumla kwa weledi na ufanisi mkubwa".
Kuhusu chama alisema hakuna miujiza itakayoiinua CCM zaidi ya kuimarisha uhai wa mashina na matawi na ni kutokana na kujua umuhimu huo, ndiyo sababu ameanza kazi kwa kufanya ziara za kuibua uhai wa chama na kutaka viongozi ngazi zote wa CCM kufuata nyayo zake.
Katika ziara hiyo Kinana ambaye anafuatana na makatibu wa NEC, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni), mbali na kukagua uhai wa matawi na mashina, pia amekuwa akifanya mikutano ya hadhara na ya ndani, akisikiliza kero za wananchi. Katika kufanya hivyo, pia amefuatana na baadhi ya mawaziri akiwamo Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri.
Akiwa Mtwara Kinana alitoa fursa kwa wananchi kueleza kwa kina kero za korosho ambapo Waziri wa Kilimo na Ushirika, Christopher Chiza alipanda jukwaani kufafanua kwa kina hali ya pembejeo za kilimo cha zao hilo ilivyo, changamoto zake na namna Serikali inavyojaribu kuzitatua. Pia Chiza alizungumzia suala la wakulima wa zao hilo kucheleweshewa malipo yao.

No comments:
Post a Comment