Friday, November 23, 2012

FAMILIA YAKUBALIANA 'KUMUUA' BONDIA CAMACHO...

Ni kwamba familia ya bondia mkongwe Hector 'Macho' Camacho jana ilitarajiwa 'kumuua' ndugu yao huyo aliye mahututi hospitalini baada ya kufikia uamuzi kuruhusu kuondolewa mashine za kupumulia zinazomsaidia kuishi, mwakilishi wa bondia huyo mkongwe ameeleza.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, familia yake ilifikia uamuzi huo baada ya madaktari kuthibitisha kwamba mfumo wake wa fahamu umekufa.
Mwakilishi huyo alisema kwa sasa familia yake inafanya maandalizi ya msiba, na wanajadiliana kuhusu mahali atakapozikwa kati ya Puerto Rico au New York.
Kama ilivyoripotiwa awali, Camacho alipigwa risasi mara kadhaa wakati walipokuwa wakipita barabarani Jumanne nchini Puerto Rico. Alikimbizwa hospitali ya jirani ambako aligundulika kupata matatizo ya moyo.
Bingwa huyo wa zamani wa ndondi aliripotiwa kuwa katika kiti cha abiria cha gari ... ndipo gari moja likawapita na kuwazuia kwa mbele na kisha mtu mmoja akaanza kuwamiminia risasi ... akimshambulia Camacho mara kadhaa shingoni na usoni.
Dereva wa gari hilo la Camacho aliuawa katika shambulio hilo. Polisi wamesema walikamata pakiti 10 za coacine kutoka kwenye gari hilo, 9 kati ya hizo zikiwa kwa dereva.

No comments: