![]() |
| Dk Abdallah Kigoda. |
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amevunja Bodi ya Shirika la Viwango (TBS) katika hatua za kuboresha utendaji wa shirika hilo.
Akizungumza baada ya kutangaza hatua hiyo jana, Dk Kigoda alisema utaratibu mwingine unaendelea ili kupata Bodi mpya haraka ambayo itaongeza tija, ufanisi na uwajibikaji katika shirika hilo.
Dk Kigoda alisema hayo Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kuvunjwa kwa Bodi hiyo na kuongeza kuwa watakuwa makini katika kuchagua Bodi mpya ili ifanye kazi itakayokidhi matakwa ya wananchi na Taifa pia.
“Utaratibu unaendelea wa kuunda Bodi mpya ambayo itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na tija na yenye kujali uwajibikaji pia,” alisema Dk Kigoda na kuongeza kuwa Bodi hiyo aliivunja juzi na haitachukua muda mrefu kuunda nyingine.
Kuhusu suala la kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS, Charles Ekelege kutokana na tuhuma Mei, alisema suala lake linafanyiwa kazi na vyombo vya Dola vya uchunguzi na kwamba litakamilika muda usio mrefu.
Hata hivyo, alisema baada ya kuundwa kwa Bodi mpya, nafasi ya ukaimu iliyopo sasa katika shirika hilo, itakwisha na kujulikana kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo ambaye atakuwa na mamlaka kamili yenye kumwezesha kutoa uamuzi. Kwa sasa nafasi hiyo inakaimiwa na Leandry Kinabo.
Bodi iliyovunjwa ina wajumbe 11 ambao ni Mwenyekiti Oliva Mhaiki, Donald Chidou (Katiba na Sheria), Rashid Salim (Viwanda na Biashara Zanzibar), Dk Bertha Maegga (Afya na Ustawi wa Jamii), Odilo Majengo (Viwanda na Biashara) na Profesa Ntengwa Mdoe (Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo-SUA).
Wengine ni Peter Machunde (Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini-TPSF), Godfrey Mariki (Tume ya Ushindani Tanzania--FCC), Suzy Laizer (SME’s), Elpina Mlaki (Fedha na Uchumi), George Simbachawene (Mbunge Kibakwe-sasa ni Naibu Waziri Nishati na Madini) na Ekelege.
Akizungumza na gazeti la Daily News, Mwenyekiti wa Bodi Mhaiki alisema anasubiri taarifa kutoka kwa mamlaka ya uteuzi wake ambayo ni Rais.

No comments:
Post a Comment