![]() |
| Philip Mangula. |
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula amesema mtumishi yeyote wa chama hicho, akihusishwa na rushwa atashughulikiwa sawia bila kusubiri Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Alitoa kauli hiyo jana katika ofisi ndogo za makao makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam wakati Sekretarieti mpya ya chama hicho ilipokabidhiwa rasmi ofisi.
“Kwenye siasa hakuna Takukuru, kama mtu ananyooshewa vidole na anaonekana ana matatizo, ikiwamo kwenda kinyume na maadili, kwa nini tuwasubiri Takukuru? Tutamchukulia hatua kwa mujibu wa kanuni na Katiba yetu,” alisema Mangula.
Alisema suala la nidhamu ni muhimu katika taasisi yoyote, kwa sababu inawezesha watu kufanya kazi vema kwa umoja na upendo na kwamba bila nidhamu, matatizo ya mitafaruku na majungu huibuka na kuharibu sifa ya chama.
“Napenda kusisitiza kuwa vitu hivi vya majungu, rushwa, ukosefu wa maadili na makundi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Nidhamu na Maadili ya Chama hiki sitovivumilia,” alisisitiza.
Pamoja na hayo, Mangula alionya wanaoanzisha makundi ndani ya chama hicho na baadhi ya wanachama kulalamika na kuwataka watumie vikao vya chama hicho kukomesha tabia hiyo.
Kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema chama kinaona ni vyema kuanzisha utaratibu mzuri wa kudhibiti wanaojitangaza kuwania urais na ubunge ili kuepusha mifarakano na makundi ndani ya chama.
“Tutandaa mfumo mzuri wa kudhibiti wanaotaka vyeo vikubwa katika uchaguzi mkuu ujao, ili wanapojitangaza tuwafuatilie, kwa sababu muhimu tu, za kukiepusha chama na matatizo ya mifarakano na rushwa,” alisisitiza.
Wakati Mangula akitoa onyo siku ya kwanza katika ofisi hiyo, kesho Sekretarieti ikiongozwa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, inatarajia kuanza ziara katika mikoa minne kufuatilia shughuli za maendeleo ikifuatana na mawaziri wa sekta husika.
Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari kwamba Sekretarieti hiyo itafanya ziara Mtwara, Rukwa, Arusha na Geita.
Alisema wataanza ziara kesho Mtwara na pamoja na mambo mengine wataangalia maendeleo ya bandari ya mkoa huo na zao la korosho linavyoendelea na mawaziri husika watatoa maelezo ya maendeleo ya sekta hizo.
Mkoani Rukwa, Sekretarieti itatembelea Mpanda na Sumbawanga ambako itafuatilia maendeleo ya sekta ya miundombinu hususan usafiri wa treni, viwanja vya ndege na barabara kwa kuwa ndio kero kubwa mkoani humo.
Ikiwa Geita Sekretarieti itafuatilia shughuli za migodini na Arusha itafuatilia ufufuaji wa viwanda katika hatua ya kukabiliana na tatizo la ajira.
“Katika ziara hii tutafuatana kote na mawaziri husika, lengo hapa ni kusimamia kwa vitendo utendaji wa Serikali sisi kama chama ambacho tumepewa dhamana na wananchi, kwa kuwa ikiboronga mwisho wa siku wa kulaumiwa ni CCM na Ilani yetu,” alisema Nape.
Alisema iwapo chama hicho kitabainika utendaji mbovu wa waziri husika ama uzembe, hakitasita kumshauri Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete aliyeteua mawaziri, kuwa hawaridhishwi na utendaji wa waziri husika.

No comments:
Post a Comment