![]() |
| Marehemu Mariam Khamis. |
Mariam alifariki jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kifafa cha uzazi alichopata mara baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa. Mtoto aliyejifungua yuko salama na kwamba anaendelea vizuri chini ya uangalizi maalumu.
Baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Sembuli, alisema kuwa wamefikia uamuzi wa kumzika marehemu leo, baada ya kuombwa na Mkurugenzi wa TOT Kapteni Komba kufanya hivyo ili wanamuziki wenzake wapate kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.
Wanamuziki wa kundi zima la taarabu la TOT wako Dodoma kutumbuiza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na kwamba msiba wa marehemu uko nyumbani kwa baba yake mkubwa Magomeni Makuti, Mtaa wa Ndovu Bar.
Mariam alitamba sana na wimbo wa Paka Mapepe alioimba akiwa na Melody, na kufanya mashabiki wake kumbatiza jina hilo, kabla ya kujiunga na bendi za Zanzibar Stars, Five Stars na hatimaye TOT ambako mauti yamemfika.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ulikuwa ni ‘Sidhuriki na Lawama’ ambao bado unashika chati katika vituo mbalimbali vya redio nchini.
Wasanii na mashabiki mbalimbali jana walijumuika katika Hospitali ya Muhimbili ulikohifadhiwa mwili wa marehemu.

No comments:
Post a Comment