Wednesday, November 14, 2012

CHEKA TARATIBU...

Watoto wa wanajeshi, Ambwene na Chacha walikuwa wakitambiana kuhusu uhodari wa baba zao jeshini. Ambwene akaanza, "Baba yangu ni Injinia. Anaweza kufanya chochote. Unaujua Mlima Kilimanjaro?" Chacha akajibu, "Ndiyo naufahamu." Ambwene akasema, "Ule umejengwa na baba yangu." Chacha hakukubali akasema, "Na wewe unaifahamu Red Sea?" Ambwene akajibu, "Ndio nimeisikia." Chacha akamalizia, "Baba yangu ndio aliua watu kisha akamwagia damu mle!" Kasheshe...

No comments: