Saturday, November 24, 2012

MWANAMKE ALIYEFANYA MAPENZI KWENYE TEKSI DUBAI AFUNGWA...

KUSHOTO: Rebecca na Conor wakiongozana na mawakili wao kuingia mahakamani. JUU: Rebecca Blake. CHINI: Conor McRedmond.
Mwanamke wa Kiingereza amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela huko Dubai ambacho kitafuatiwa na adhabu ya kurejeshwa kwao kwa kosa la kufanya ngono huku wakiwa wamelewa katika kiti cha nyuma cha teksi jijini humo.
Rebecca Blake mwenye miaka 29, alikamatwa mapema mwaka huu baada ya kuvua nguo nusu nyuma ya teksi baada ya kuwa akinywa pombe kwa masaa kumi.
Raia wa Ireland, Conor McRedmond mwenye miaka 28, ambaye walikamatwa naye, pia alipatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu kama hiyo, licha ya majibu ya kipimo cha DNA kutoonesha muingiliano wowote kati ya wawili hao.
Wawili hao wameachiwa kwa dhamana wakisubiria kusikilizwa kwa pingamizi lao Januari, mwakani lakini watalazimika kusherehekea Krismasi mjini Dubai sababu wamenyang'anywa pasi zao za kusafiria.
Mshauri wa mambo ya ajira, Rebecca anayetokea Dorking huko Surrey, alikamatwa Mei 4 baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na Conor masaa machache tu kabla.
Dereva wa teksi yao aliwatonya polisi baada ya kumwona Rebecca katika kioo cha kutazama nyuma akiwa kavua nguo zake za juu, akipapasana na Conor huku 'akitoa sauti ya mwanamke anayefanya mapenzi'.
Rebecca, ambaye alihamia Dubai Septemba mwaka jana kuchukua nafasi hiyo ya kazi kwa malipo ya mshahara wa Pauni za Uingereza 100,000 kwa mwaka kwenye kampuni ya kusaka ajira ya Manpower, alikuwa akinywa katika Hoteli ya Rotana. Hapo kabla alisema: "Walikuwa wakiendelea tu kunijazia glasi yangu."
Ilipofika Saa 10 jioni, alihamia katika baa ya hoteli hiyo na kufurahia wakati wa furaha hadi Saa 12 jioni kabla ya kuendelea kunywa katika Pub ya Irish Village akiwa na Conor.
Rebecca, ambaye alikiri kunywa glasi nne za vodka na glasi tano za mvinyo, kisha akapanda teksi majira ya Saa 4:30 usiku akiwa na Conor, kutoka County Offaly, ambako alikuwa amekunywa glasi 'sita au saba' za kinywaji cha vodka.
Dereva wa teksi raia wa Pakistan, Qaiser Khan mwenye miaka 29, aliieleza mahakama katika maelezo yake wawili hao walionekana kuchanganyikiwa na Conor alikunywa pombe kwenye chupa.
Alisema: "Nilimweleza hairuhusiwi kunywa pombe ndani ya teksi.
"Kilichofuata, nilitazama kwenye kioo na kuona mwanamke akiwa amemkalia mwanaume mapajani. Alikuwa mtupu, akipanda na kushuka huku akitoa sauti."
Khan alisema aliongeza mwendo na kuona polisi wa doria na kumwita ofisa wa Emirati, Abdullah Obaid Khamis mwenye miaka 22, ambaye ambaye alisemekana kuwaona wawili hao bado wakiendelea kufanya ngono.
Abdullah alisema: "Mwanaume alikuwa kifua wazi, suruali yake ilikuwa imeshushwa chini ya magoti na mwanamke hakuwa amevaa nguo ya ndani."
Dereva teksi alidai Rebecca aliahidi kumpa 'kiasi kikubwa cha pesa' kuwaeleza waendesha mashitaka kwamba wawili hao walikuwa wakibusiana na sio kufanya ngono lakini alikataa.
Wakili wa utetezi wa wapenzi hao alisema kuna vitu vinatofautiana katika ushahidi. Pia alisema wapenzi hao hawawezi kuwa walikuwa wakifanya ngono sababu Rebecca alikuwa katika siku zake, akaongeza: "Hii ni Dubai, sio msikiti. Kila mmoja anakunywa pombe."
Rebecca na Conor walikanusha kufanya ngono na kukosa heshima. Awali walipatikana na hatia ya kutumia pombe na walitozwa faini ya Pauni za Uingereza 512.
Wote walisema hawana cha kusema.
Wamekuwa wataalamu wa mwishoni kupatikana na hatia katika sheria kali za Umoja wa Falme za Kiarabu kuzuia ulevi wa hadharani na kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Mwaka 2008, Vince Acors mwenye miaka 38, na Michelle Palmer mwenye miaka 40 walifungwa jela miezi mitatu kwa kufanya ngono katika ufukwe. Hukumu hiyo ilisitishwa kufuatia pingamizi lililowekwa.
Na mwaka 2009, Charlotte Adams na Ayman Najafi walitumikia mwezi mmoja jela baada ya mwanamke wa Emirati kudai walikuwa wakibusiana hadharani.

No comments: