![]() |
| Bondia Camacho akiwa katika mashine za kumsaidia kupumua muda mfupi kabla ya kutangazwa kafariki dunia jana. |
Hector 'Macho' Camacho, bondia wa Puerto Rico anayefahamika kwa utaalamu wake ulingoni na pia kwa maisha yake ya gharama, ametangazwa kufariki dunia jana Jumamosi ikiwa ni siku nne baada ya kupigwa risasi usoni. Alikuwa na umri wa miaka 50.
Akipigwa risasi wakati ameketi katika gari lililoegeshwa nje ya baa Jumanne iliyopita akiwa na rafiki yake katika Jiji la Bayamon, alitangazwa kufa kwenye kituo cha Centro Medico mjini San Juan. Rafiki yake aliyekuwa naye mwenye miaka 49, Adrian Mojica Moreno, alikufa papo hapo katika eneo la tukio.
Polisi walisema Mojica alikuwa na pakiti ndogo tisa za dawa za kulevya aina ya cocaine na pakiti ya kumi ilikuwa iko wazi ndani ya gari hilo.
Camacho ambaye asili yake ni kutoka Bayamon, nje kidogo ya San Juan, aliaminika kama taswira ya kipaji halisi, na bondia aliyeiva kimafunzo ambaye pengine alifunikwa na mazuri ya mpinzani wake wa muda mrefu, nyota wa Mexico Julio Cesar Chavez, ambaye alimpiga katika pambano lililosubiriwa kwa muda mrefu mjini Las Vegas mwaka 1992.
Camacho alipigana katika ngumi za kulipwa kwa miongo mitatu, tangu pambano lake gumu dhidi ya David Brown kwenye ukumbi wa Felt Forum mjini New York mwaka 1980 sawa na ilivyokuwa kwa lile lisilosahaulika dhidi ya Sal Duran huko Kissimmee, mjini Florida mwaka 2010.
Kipindi cha katikati, amepambana na baadhi ya nyota wakubwa kwa enzi mbili, akiwamo Sugar Ray Leonard, Felix Trinidad, Oscar De La Hoya na Roberto Duran.
Juzi Ijumaa, mama wa Camacho alikaririwa akisema kwamba mashine za kumsaidia kupumua mwanae lazima zifikie ukomo na hivyo kesho (jana Jumamosi) zitamwa rasmi.
Camacho alipigana kwa mara ya mwisho Mei mwaka 2010 ambapo alipigwa Duran.
Ameacha rekodi nzuri kwa kushinda mapambano 79, kupoteza 6 na kutoka sare matatu.

No comments:
Post a Comment