Friday, November 23, 2012

MSANII MLOPELO WA KUNDI LA KAOLE AFARIKI DUNIA...

Msanii maarufu wa kundi la maigizo la Kaole, Mlopelo amefariki dunia jana katika Hospitali ya Temeke baada ya kuwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kwa muda mrefu.
Mlopelo ambaye alijipatia umaarufu kutokana na kuigiza filamu nyingi za kishirikina akishirikiana na msanii mwenzake wa kundi hilo, Bi Mwenda, anatarajiwa kuzikwa leo Saa 4 asubuhi kwenye makaburi ya Wailes, Temeke jijini Dar es Salaam.
Ifuatayo ni kipande cha mahojiano aliyofanya marehemu Mlopelo na Mtangazaji Zamaradi Mketema wa kipindi cha TakeOne cha Clouds Tv hivi karibuni.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Mlopelo.

No comments: