Thursday, November 22, 2012

BONDIA HECTOR CAMACHO YU MAHUTUTI BAADA YA KUMIMINIWA RISASI...

KUSHOTO: Hector 'Macho' Camacho akiwa mahututi hospitalini. KULIA: Muda mfupi baada ya tukio huku mwili wa Moreno ukiwa umetelekezwa chini.
Takribani pakiti 10 za dawa za kulevya aina ya cocaine zimekutwa eneo ambalo bondia mkongwe Hector 'Macho' Camacho alipigwa risasi jana, hii ni kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini Puerto Rico.
Polisi wamesema ... rafiki wa Camacho, ambaye alikuwa akiendesha gari walilokuwa wakisafiria, alikuwanazo pakiti 9 kati ya hizo za cocaine ... na pakiti ya kumi ilikuwa wazi wakati zilipopatikana.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Camacho na rafiki yake Adrian Mojica Moreno walishambuliwa kwa risasi na watu waliojificha kwenye gari lililokuwa limeegeshwa kando wakati wakipita na gari lao aina ya Ford Mustang katika eneo la San Juan.
Moreno alifariki dunia katika eneo la tukio ... na Camacho -- ambaye alipigwa risasi mara kadhaa usoni na shingoni -- alikimbizwa kwenye hospitali ya karibu ambako alipatwa na mshituko wa moyo.
Mwakilishi wa Camacho alieleza, bondia huyo hajitambui na madaktari wamesema anahitaji muujiza kuweza kupona.

No comments: