![]() |
| Jon Bon Jovi akiwa na binti yake, Stephanie. |
Binti wa Jon Bon Jovi mwenye miaka 19, Stephanie Rose Bongiovi amekamatwa chuoni anakosoma huko Upstate New York mapema jana asubuhi baada ya kutuhumiwa kujizidishia dozi ya dawa za kulevya aina ya heroin, imefahamika.
Kwa mujibu wa Idara ya Polisi ya Town of Kirkland, polisi walivamia chumba chake katika Chuo cha Hamilton baada ya mtu mmoja kuripoti kwamba Stephanie anadaiwa kujizidishia dozi ya heroin na alikuwa hajitambui.
Sambamba na polisi, madaktari wa huduma za dharura pia walifika eneo la tukio na kumkuta Stephanie akiwa hai.
Polisi wamesema kikosi cha kupambana na dawa za kulevya kilipekua eneo la tukio na kukuta 'kiasi kidogo' cha heroin ... pamoja na mihadarati sambamba na vikorokoro vya dawa za kulevya - yote makosa madogo.
Stephanie baadaye aliachiwa kutoka rumande - na kuamriwa kuripoti mahakamani katika siku zijazo.
Mwanafunzi mwingine pia alikamatwa - mvulana wa miaka 21 ambaye pia alishitakiwa kwa kupatikana na dawa za kulevya.
Stephanie ni binti pekee wa Jovi na ndiyo mkubwa kati ya watoto wanne aliozaa na mkewe Dorothea Hurley.

No comments:
Post a Comment