![]() |
| Ndege mpya ya FastJet katika hatua za mwisho kabla ya kuanza rasmi safari zake Alhamisi ijayo. |
Hakuna namna nyingine ya kuelezea kwa ufasaha, ila kwa kifupi unaweza kuiita "Basi la Angani". Hii si nyingine bali ni ndege mpya ya FASTJET ambayo inatarajiwa kuanza rasmi kuliteka anga la Tanzania Alhamisi ijayo ya Novemba 29, 2012 ikianza kwa safari za DAR-MWANZA na DAR-K'NJARO. Tunasema "Basi la Angani" kutokana na ukweli kwamba tofauti na ilivyozoeleka kwa usafiri wa anga ni gharama kubwa kulinganisha na usafiri wa barabara, FastJet imeleta mapinduzi makubwa hasa kwa upande wa nauli. FastJet imekuja kuwawezesha watu wa kipato cha chini kuweza kuweka historia kwa kuweza kupanda ndege kwani inatoza nauli sawa na zile za kwenye mabasi na pengine chini kidogo. Huwezi kuamini, sasa unaweza kwenda Kilimanjaro kwa nauli ya Shilingi 32,000/- tu! Timiza ndoto yako, kuwa wa kwanza Alhamisi ijayo kupanda ndege mpya ya FastJet ambapo unaweza kufanya Booking kupitia mtandao wao wa www.fastjet.com.

No comments:
Post a Comment