![]() |
| KUSHOTO: Walipakodi wa Uingereza wakiandamana kupinga madai ya Qatada. KULIA: Abu Qatada akitoka nyumbani kwake. |
Mtuhumiwa wa ugaidi, Abu Qatada ameieleza familia yake kwamba amepanga kuishitaki Serikali ya Uingereza kudai fidia ya Pauni za Uingereza milioni 10 kwa 'kwa kushikiliwa kinyume cha sheria'.
Mhubiri huyo anayepigwa vita amesema anataka fidia kwa 'kutendewa visivyo' baada ya Jaji kumwachia huru kutoka jela wiki iliyopita na kuzuia kurejeshwa kwake nchini Jordan kujibu mashitaka ya ugaidi.
Qatada alitunukiwa malipo kiduchu kutoka Mahakama ya Ulaya inayoshughulikia Haki za Binadamu miaka mitatu iliyopita baada ya majaji kuamua kwamba alikuwa akishikiliwa kimakosa kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh bila kufunguliwa mashitaka.
Lakini familia ya mfuasi huyo wa dini ilisema kwamba matumaini yake ya kupata fidia kubwa zaidi yamechagizwa baada ya mahakama maalumu ya uhamiaji kuamua Jumatatu iliyopita kwamba kulikuwa na hatari dhahiri kwamba ushahidi uliopatikana kupitia mateso unaweza kutumika dhidi yake endapo angerejeshwa nchini Jordan kukabiliana na mashitaka.
Mfuasi huyo wa dini, ambaye aliwahi kuelezewa na jaji kama Balozi wa Osama Bin Laden barani Ulaya, amewekewa dhamana kwa familia yake mjini London baada ya kutumia zaidi ya miaka yake saba iliyopita akiwa gerezani.
Qatada anaishi North London pamoja na mkewe na watoto wake watano katika nyumba aliyokabidhiwa na jimbo hilo inayosemekana kugharimu Pauni za Uingereza 1,000 kwa mwezi.
Kaka yake, Ibrahim Othman alisema: "Alisema anatumaini kupata Pauni za Uingereza milioni 10 kwa kuswekwa jela kimakosa.
"Anasema atawasilisha madai yake wakati taratibu za mahakama zitakapomalizika kwa kutendewa visivyo.
"Hakufanya chochote kibaya dhidi ya watu wa Uingereza lakini Mamlaka za Uingereza zikamtupa gerezani kwa miaka mingi.
"Hakufunguliwa mashitaka yoyote nchini Uingereza. Ni sahihi kwamba lazima alipwe fedha hizo.
"Hakuweza kufanya kazi kwa kipindi kirefu sababu alikuwa gerezani, hivyo anawezaje kujikimu bila kulipwa fidia wakati yote sasa yameisha?"
Othman alisema kwamba kama Qatada angefanikiwa alitarajia kutumia fedha hizo kununua nyumba mpya nchini Jordan, endapo angeruhusiwa kurejea bila kushitakiwa, na pia kuwekeza katika Taasisi ya Kiislamu kusaidia watu masikini nchini humo. Kushindikana kurejeshwa Qatada kumewagharimu walipakodi zaidi ya Pauni za Uingereza milioni 3, ikiwamo Pauni za Uingereza 500,000 kwa upelelezi.
Chini ya masharti ya dhamana yake, anaruhusiwa kutoka nje kati ya Saa 2 asubuhi na Saa 10 jioni, ambapo katika muda huo atakuwa akifuatiliwa kwa karibu na polisi. Pia hawezi kuongoza sala, kutoa mihadhara, kuhubiri au kutoa maelekezo ya kidini isipokuwa tu kwa mkewe na watoto nyumbani.
Othman alisema Qatada alimpigia simu mama yake kutoka Amman, mji mkuu wa Jordan, Jumatatu jioni, masaa kadhaa baada ya ushindi wake kortini.
Alisema: "Kaka yangu alisema alikuwa na furaha mno kwa ushindi wake. Bado anataka kurejea nchini Jordan, lakini tu akiwa mtu huru. Atafungua kesi kwa ajili ya kudai fidia pale atakaposafishwa kabisa na mahakama, kitu ambacho ana uhakika kabisa kitafanyika."
Qatada alitunukiwa Pauni za Uingereza 2,500 na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu mwaka 2009 baada ya kufunguliwa kesi pamoja na watuhumiwa wengine 10 wa ugaidi ambao walishikiliwa bila kushitakiwa chini ya sheria za ugaidi zilizoanza kutumika baada ya mashambulio ya Septemba 11.
Mahakama ilisema masharti ya kushikiliwa kwake yamekiuka vipengele vitatu vya Mkataba wa Haki za Binadamu.
Mapema wiki hii majirani wa mhubiri huyo anayepigwa vita walikasirishwa mno kusikia kwamba Qatada anataka kuhamishiwa kwenye nyumba kubwa itakayolipiwa na walipakodi.
Mhubiri huyo mwenye miaka 52 anaaminika amewasilisha ombi hilo akieleza anakata nafasi kubwa zaidi kwa ajili ya mke wake na watoto.
Lakini wakazi hao walisema wamekerwa na madai ya Qatada. Mmoja mama wa watoto wawili, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema: "Unataka kuwa gaidi sasa ili kupata nyumba kubwa? Tayari ana nyumba ya vyumba vitano vya kulala."

No comments:
Post a Comment