Tuesday, November 20, 2012

CHEKA TARATIBU...

Kibaka kaingia kanisa moja la walokole. Ulipofika wakati wa kutoa sadaka Kibaka yule akawa wa mwisho kabisa kwenda kwenye kikapu ya kukusanyia sadaka. Badala ya kuweka pesa, yule Kibaka akazoa noti kadhaa za Shilingi 10,000. Mchungaji akamkamata na kuwataka waumini wasimdhuru kwanza sababu wamepokea wokovu. Mchungaji akamuuliza, "Kwanini unaiba fedha tulizomtolea Mungu?" Yule Kibaka kwa kutumia mwanya huohuo akajibu, "Ni kweli mmemtolea Mungu, na mimi nimemuomba Mungu ndio akaniruhusu nichukue!" Kasheshe…

No comments: