![]() |
| Katibu Mkuu mpya wa CCM, Abdulrahman Kinana. |
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa kikao cha NEC ya Chama Cha Mapinduzi kinachoendelea mjini Dodoma muda mfupi uliopita kimefanya uteuzi wa sekretarieti mpya ya chama hicho.
Katika uteuzi huo, Abdulrahman Kinana anakuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Wilson Mukama.
Wengine walioteuliwa ni Ali Vuai Ali anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Dk Mwigulu Nchemba anakuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, wakati Nape Nnauye anaendelea na wadhifa wake wa Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Nafasi ya Katibu wa Fedha na Uchumi sasa itashikwa na Zakia Meghji, wakati Katibu wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa anakuwa Dk Asha-Rose Migiro na Mohammed Seif Khatib anakuwa Katibu wa Oganaizesheni.

Taarifa zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.

No comments:
Post a Comment