Thursday, November 15, 2012

MLOLONGO WA MATUKIO YA MTUHUMIWA WA UGAIDI UINGEREZA...

Abu Qatada akishuka kwenye gari mara baada ya kuachiwa huru kutoka gereza lenye ulinzi mkali nchini Uingereza.
Abu Qatada amekuwa akitajwa kama kiongozi wa kiroho wa Al Qaeda huko Ulaya, mhubiri muhimu wa siasa kali nchini Uingereza na 'mtu hatari mno'.
Tangu mwaka 2001, wakati wa hofu ya tishio la ugaidi wa ndani ilipoibuka kufuatia mashambulizi ya Septemba 11, alihoji kila jaribio la Serikali kumkamata na kumrejesha kwao.
Yafuatayo ni matukio muhimu kuhusu mapambano yake ya muda mrefu kukabiliana na jaribio la kumtimua.
1993: Baba huyo wa watoto watano rais wa Jordan, ambaye jina lake halisi Omar Mahmoud Mohammed Othman, aliomba hifadhi ya ukimbizi wakati alipowasili nchini Uingereza kwa pasipoti ya kughushi.
1994-June: Anakubaliwa kuishi nchini Uingereza.
1995-Machi: Qatada anaruhusu 'fatwa' inayoruhusu mauaji ya wote wanaojiengua kutoka Uislamu, wake zao na watoto nchini Algeria.
1998-Mei: Anaomba ruhusa ya kubaki nchini Uingereza kwa muda usiojulikana.
1999-Aprili: Anatiwa hatiani kwa mashitaka ya ugaidi nchini Jordan licha ya kutokuwepo mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
1999-Oktoba: Mtuhumiwa huyo azungumza mjini London akitetea mauaji ya Wayahudi na kubariki mashambulizi dhidi ya Wamarekani.
2001-Februari: Anakamatwa na polisi wa kuzuia ugaidi kwa kujihusisha katika mpango wa kulipua Soko la Krismasi la Strasbourg. Maofisa wanamkuta akiwa fedha taslimu Pauni za Uingereza 170,000, zikiwamo Pauni 805 kwenye bahasha iliyoandikwa juu yake 'Kwa mujahidina mjini Chechnya'.
2001-Desemba: Anakuwa mmoja wa watu wanaosakwa vikali baada ya kutoweka kutoka nyumbani kwake huko Acton, West London.
2002-Oktoba: Anakamatwa na polisi katika nyumba ya halmashauri iliyoko kusini mwa London na kushikiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh.
2005-Machi: Anaachiwa huru kwa dhamana na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu.
2005-Agosti: Mhubiri huyo anakamatwa chini ya sheria za uhamiaji wakati Serikali ikiwa katika harakati za kumrejesha nchini Jordan.
2008-Aprili: Mahakama ya Rufani yaamua kwamba kumrejesha kwao Qatada ni kuvunja haki za bianadamu sababu ushahidi uliotolewa dhidi yake nchini Jordan unawezekana ulipatikana kutokana na mateso.
2008-Mei: Qatada anapewa dhamana na mahakama ya uhamiaji lakini anaambiwa lazima ajifungie ndani masaa 22 kwa siku.
2008-Juni: Anaachiwa huru kutoka gereza ka Long Lartin huko Worcestershire na kwenda kuishi kwenye nyumba ya vyumba vine vya kulala yenye thamani ya Pauni za Uingereza 800,000 iliyoko magharibi mwa London.
2008-Novemba: Nakamatwa tena baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani kulieleza baraza la usikilizwaji shauri hilo la uhamiaji hofu kwamba amepanga kutoroka.
2008-Desemba: Dhamana ya Qatada yatenguliwa na Kamisheni Maalumu ya Rufani za Uhamiaji (SIAC) baada ya kusikiliza ushahidi wa siri kwamba hatari ya yeye kutoroka imeongezeka.
2009-Februari 19: Qatada anatunukiwa Pauni za Uingereza 2,500 kama fidia na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu baada ya majaji kuamua kwamba kushikiliwa kwake bila kufunguliwa mashitaka nchini Uingereza chini ya nguvu ya kuzuia ugaidi kumevunja haki zake za binadamu.
2012-Februari 6: SIAC yaamua anaweza kuachiwa kwa dhamana, licha ya kuwepo hatari kwa usalama wa taifa.
2012-Februari 9: David Cameron na King Abdullah wa Jordan wakubaliana juu ya 'umuhimu wa kutafuta suluhisho la kudumu' katika kesi yake, Downing Street imesema.
2012-Februari 13: Yabainika kwamba Qatada ameachiwa kwa masharti magumu ya dhamana kutoka katika gereza la Long Lartin.
2012-Aprili 17: Anakamatwa huku Serikali ikijiandaa kumrejesha nchini Jordan, wakati Rais wa SIAC, Justice Mitting akisema Waziri wa Mambo ya Ndani Theresa May amehakikisha uhakika kutoka Jordan kwamba itahakikisha Qatada anahukumiwa kwa haki.
2012-Aprili 18: Timu ya wanasheria wa Qatada wawasilisha pingamizi jipya na majaji wa haki za bianadamu Ulaya, ikisema mahakama yenye makao yake Strasbourg ilikosea pale ilipoamua kwamba hawezi kuwa katika hatari ya mateso kama akirejeshwa. Waziri wa Mambo ya Ndani alisisitiza uamuzi huo ni 'njama za kuchelewesha' nakudai kwamba rufani ilichelewa mno kuweza kukubalika kwa vyovyote vile.
2012-Aprili 30: Tawi la Al Qaida la Afrika Kaskazini, al Qaida katika Maghreb ya Kiislamu, imetoa ofa ya kumwachia huru Stephen Malcolm endapo Qatada ataachiwa na Uingereza.
Siku hiyohiyo, aliyekuwa Waziri wa Uhamiaji Damian Green asema majaribio kadhaa yaliyoshindwa kumrejesha Qatada yamegharimu Pauni za Uingereza 825,000 katika ada za kisheria tangu mwaka 2002 na kuthibitishwa kwamba gharama hiyo itazidi kuongezeka.
2012-Mei 9: Qatada anapoteza katika jaribio lake la kutaka rufani yake dhidi ya kurejeshwa kusikilizwa na Korti Kuu ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, ikisafisha njia mipango ya kurejeshwa kuendelea. Hukumu hiyo ilikwepwa katika upenyo mdogo sana kwa May, wakati wakitupa kesi, jopo la majaji watano pia likiamua kwamba rufani ya Qatada katika usiku wa Aprili 17 lilikuwa ndani ya muda wa mwisho wa mahakama.
2012-Mei 28: Jaribio la mtuhumiwa huyo la kutaka uhuru linazuiwa na Rais wa SIAC Justice Mitting huku akikataa dhamana, akisema kwamba kumwachia Qatada katika mitaa ya London ingeweza kuwa tatizo kubwa kiulinzi katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki.
2012-Agosti 9: Qatada ashindwa ombi jipya la kutaka uhuru kwenye Mahakama Kuu, wakati majaji wakitupilia mbali kwamba kungekuwa na mwaka mwingine au zaidi wa kufungua madai kabla uamuzi wa mwisho kutolewa.
2012-Oktoba 10: Kusikiliwa ka rufani ya Qatada, ambayo itapima uhakika uliotolewa na Jordan, inasikilizwa na Rais wa SIAC Justice Mitting, Jaji wa Mahakama ya juu Peter Lane na Dame Denise Holt.
2012-Novemba 12: SIAC yaruhusu rufani yake.

No comments: