Monday, October 8, 2012

BINTI ALIYETOROSHWA GAMBIA AOKOTWA UINGEREZA...

KUSHOTO: Moja ya mitaa ya Banjul ambako binti huyo alinyakuliwa. JUU: Kituo cha Roe Farm Lane ambako binti alitelekezwa. CHINI: Mtaa mbao binti huyo alitembea kwa zaidi ya dakika 40 kabla ya kuanza kuulizia njia.
Binti ambaye alinyakuliwa kutoka mtaani barani Afrika miaka mitatu iliyopita ameonekana kiajabu mjini Derby.
Polisi wamesema binti huyo mwenye miaka 17 alitelekezwa na mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari la rangi ya bluu ambaye alimweleza 'aende katika kituo cha polisi kilicho jirani.'
Baada ya kupata msaada kwa mpita-njia, binti huyo, ambaye hakutajwa jina lake, alikwenda kituo cha treni cha Roe Farm Lane huko Chaddesden.
Binti huyo aliwaleza maofisa wa polisi alitekwa nyara huko Banjul, mji mkuu wa Gambia, wakati akiwa anatoka shule mwaka 2009 na kuwa alisafirishwa kwenda Uingereza muda mfupi baadaye, kupitia Ufaransa.
Lakini alisema hakuwa na akifahamu ni wapi alipokuwa akishikiliwa wakati akiwa Uingereza, kwa mujibu wa Mpelelezi Inspekta Paul Tatlow, ambaye anajaribu kutafuta kama pengine ilikuwa ni Derbyshire.
Inspekta Tatlow alisema binti huyo alitelekezwa kando ya barabara huko Chaddesden Alhamisi mchana na mtu na aliwasili kituo cha jirani cha polisi majira ya saa 12 jioni ya siku hiyo.
Inspekta Tatlow alisema kesi ilikuwa 'si ya kawaida' kwa watu walio chini yake.
'Katika hatua hii ya awali, hatufahamu kwanini mtu huyu alichagua kumleta binti Derby, kama alikuwa pia akiishi Derbyshire hapo kabla, au kama kulikuwa na uhusiano wowote na jiji hilo," alisema
"Tangu siku ya kuzaliwa na taarifa alizotupatia mpaka sasa, tunaamini alinyakuliwa kutoka mitaa ya mji wa Banjul, Gambia, akiwa anatoka shule miaka mitatu iliyopita.
"Kisha akaletwa Uingereza kupitia vituo kadhaa Ulaya, ikiwamo Ufaransa. Lakini binti huyo hana kumbukumbu ni wapi alikuwa akiishi kwa kipindi chote hicho cha miaka mitatu iliyopita.
"Japo uchunguzi wetu bado unaendelea, hatuamini kwamba aliletwa nchini kufanya kazi ya ukahaba."
Maofisa wanajaribu kujua nyendo za binti huyo mjini Derby na kujua gari na dereva, ambaye ni mtuhumiwa wa utekwaji nyara wake.
"Tunafahamu kutokana na kuzungumza naye kwamba watu saba au nane ambao aliongeza nao mjini Chaddesden walijitolea kumsaidia," alisema Tatlow.
"Baadhi walimwambia angeweza kutumia simu zao za mikononi sababu, kwa kufanya hivyo, polisi wangemfuata alipo. Lakini tunafahamu alielezwa na mtu huyo aliyemtelekeza kuuliza njia ya kuelekea kituo cha polisi na kwamba alikuwa akitaka kufanya hivyo.
"Kwa sasa, tunajaribu kutafuta zaidi hasa ni sehemu gani katika Derby alikotelekezwa. Alitueleza alitembea kwa takribani dakika 40 kabla ya kuanza kuuliza watu kilipo kituo cha polisi.
"Kwetu, tunafuatilia kwa ukaribu sana, kujaribu kujua nyendo zake tangu wakati alipowasili kwenye kituo cha treni cha Roe Farm."

No comments: