Monday, October 8, 2012

BAADA YA AJALI, MPENZI WA BOBBI KRISTINA AIBUKA NA KITU KIPYA...

Rafiki wa kiume wa Bobbi Kristina, Nick Gordon, amepata gari jingine jipya kabisa kufuatia ajali mbaya aliyopata na gari lake mwezi uliopita ...na unachotakiwa kufahamu ni kwamba amechukua gari kama lile lililopata ajali.
Ilivujishwa kwamba Nick na Bobbi walipata ajali mwezi uliopita akiwa anaendesha gari lake aina ya Chevy Camaro ambalo liliharibika vibaya sana huku bampa likiwa limenyofoka kabisa na tairi la mbele likiwa halijulikani liliko.
Taarifa kuhusu ajali hiyo bado hazijawa wazi, lakini imeelezwa uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea.
Kwa sasa, vyanzo vilivyo karibu na Nick vimeeleza ...hakupoteza muda kubadili gari ...na licha ya kwamba roho yake inapenda sana Maserati, haraka akaamua kuchukua Camaro mpya, kama ilivyo ile ya zamani.

No comments: