Monday, August 20, 2012

MWONGOZAJI FILAMU MKONGWE AJITUPA DARAJANI NA KUFA...


Mwongozaji filamu maarufu Tony Scott ambaye aliongoza filamu ya "Top Gun" kati ya filamu nyingi kubwa, amejirusha na kufa kwenye daraja mjini Los Angeles usiku wa kuamkia leo, imefahamika.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Ridley,  Scott mwenye miaka 68 aliruka kutoka kwenye Daraja la Vincent Thomas linalounganisha San Pedro na Kisiwa cha Terminal majira ya Saa 4:30 usiku wa kumkia leo.
Msemaji wa walinzi wa fukwe za Marekani Luteni Jennifer Osburn alisema wamekuta ujumbe ndani ya gari za Scott aina ya Toyota Prius, ambalo liliegeshwa kwenye moja ya njia za daraja hilo.
Scott aliongoza film kasha kama "Top Gun", "Beverly Hills Cop II", "Enemy of the State", an "The Taking of Pelham 123". 
Mamlaka zililazimika kutumia vifaa maalumu kutafuta mwili wa Scott ndani ya maji. Mwili wake ulipatikana majira kama ya 8:30 usiku wa manane, ikiwa ni karibu masaa manne tangu ajirushe.

No comments: