Mzimu wa madaraka umeingia katika Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki, ambapo viongozi wameanza kufukuzana kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mali za Kanisa na ukiukaji Katiba.
Kiongozi anayedaiwa kuandikiwa barua ya kuondolewa katika nafasi yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Jimbo hilo, Mchungaji Clement Fumbo. Makao Makuu ya Jimbo hilo yako Dar es Salaam.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wiki zaidi ya moja sasa, umebaini kuwa mgogoro huo uliibuka rasmi Aprili wakati Mchungaji Fumbo alipokwenda likizo ya masomo na barua ya kusimamishwa kwake kuandikwa Julai 31.
Barua hiyo inadaiwa kuandikwa na viongozi wa chini ya Mwenyekiti kimadaraka wakati Katiba ya Kanisa inatamka, kuwa Mkutano Mkuu wa Kanisa unaofanywa mara moja kwa miaka minne (ujao ni mwaka 2014), ndio una mamlaka ya kumsimamisha uongozi Mwenyekiti.
Kwa mujibu wa Katibu wa Umoja wa Mabaraza ya Wazee wa Jimbo hilo, Nelson Ngajilo, sababu zilizobainishwa katika barua hiyo ni mbili; kutopatana na viongozi wenzake wa Kamati Tendaji na Kamati Kuu na kushindwa kusimamia Katiba na mali za Kanisa.
"Baada ya kutafiti kwa kina, tulibaini kuwapo wachungaji wachache wanaoharibu Kanisa, tuliwaandikia wafafanue kwa vielelezo tuhuma za Mwenyekiti Fumbo, lakini walishindwa, tunajua nia yao ni kuweka uongozi wao kwa nguvu za pesa zao, hili si sawa," alisema Ngajilo.
Mchungaji Fumbo jana alikiri kuwapo kutoelewana baina ya viongozi, lakini alidai kutokabidhiwa barua yoyote ya kusimamishwa uongozi na anaendelea kwenda ofisini kufanya kazi na wenzake kama kawaida.
"Sijajua ni kitu gani kinaendelea katika Kanisa, nilikuwa masomoni kuandika Shahada yangu ya Uzamivu (PhD), nikasikia maneno yasiyo na ukweli, mimi nipo ofisini hata ukija utanikuta, sijakabidhiwa barua yoyote mpaka sasa," alisema Mchungaji Fumbo.
Alisema wapo watu wachache wenye kutaka kuharibu Kanisa, lakini yeye atasimamia ukweli na haki ya waumini anaowaongoza na hatasita kuzuia kiongozi kufanya jambo ikiwa halina maslahi kwa Kanisa.
Taarifa zilizopatikana hivi karibuni, zilidai kuwa baadhi ya viongozi walipanga kumwondoa Mwenyekiti huyo madarakani, ili wamweke mtu wao kwa lengo la kuwezesha mambo yao kufanyika, ikiwa ni pamoja na kufanya biashara kwa mgongo wa Kanisa.
Aidha, inadaiwa Mchungaji Fumbo alipokuwa likizo ya masomo, Makamu Mwenyekiti Mchungaji Saul Kajula alikaimu nafasi ya uenyekiti na hadi jana hajataka kuiachia. Hakupokea simu alipopigiwa.
Katika kunusuru hali hiyo, hivi karibuni uongozi wa Umoja wa Mabaraza ya Wazee jimboni humo uliandika barua kwa uongozi wa Jimbo la Kusini (Jimbo Mama) kuomba kukutana nao na kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee, Balozi David Mwaikambo juzi alisambaza ujumbe wa simu (tunao) ukiwataka viongozi wa wazee na waumini wa shirika zote za jimbo kufika katika mkutano siku ya Iddi Pili, kujua mustakabali wa suala hilo.
Mmoja wa wajumbe wa halmashauri anayetajwa kuchochea vurugu kwa nguvu za fedha ni Yona Sonelo na alipoulizwa, alidai wanaosema hayo ni wahuni, kwa kuwa uamuzi wowote wa Kanisa unafanywa kwenye vikao na si vinginevyo.
Taarifa zinaeleza pia kuwa, Rais wa Moravian duniani, Askofu Dk Paul Gardner, kupitia mitandao ya intaneti, alifikishiwa taarifa hizo na anasubiriwa kuchukua hatua.

No comments:
Post a Comment