Wednesday, August 22, 2012

ALIYETAKA KUJITUPA GHOROFANI SASA KUUAWA KWA KUPIGWA RISASI...

Hili ni tukio la kushangaza kwamba familia, marafiki na wafanyakazi wa uokoaji walihaha kujaribu kuzuia mwanamke asijitupe na kufa.
Walilazimika kuinasa miguu ya Sheng Fi ambaye alikuwa akitishia kujitupa kutoka jengo la ghorofa tisa.
Lakini kitu ambacho hawakufahamu ni kuwa alimkaba na kumtupa binamu yake mwenye miaka minne masaa kadhaa kabla na kuutupa mwili wake kutoka sehemu hiyo hiyo huko Kusini mwa China.
Sheng alikuwa ana chuki kubwa na wifi yake, mama wa mtoto huyo wa kiume ikiwa ni matokeo ya ugomvi kati yao.
Alikiri kumkaba roho hadi kufa na kuutupa mwili wake kutoka jengo hilo lenye urefu wa futi 100 mjini Zhanjiang, katika Jimbo la Guangdong kabla ya kujaribu kuruka kumfuata.
Akiwa hawajui kinachoendelea, wafanyakazi wa uokoaji, ambao waliitwa baada ya Sheng kuonekana juu ya paa, walimleta binti yake kumsihi ashuke chini ambapo wakatumia mwanya huo kumnasa na kuvuta kutoka sehemu aliyokuwa amekaa kabla ya hajatekeleza azma yake ya kujitupa.
Ukweli kuhusu sababu za kutaka kujiua ziliwekwa bayana baada ya kuondolewa kutoka kwenye ncha ya jengo hilo.
"Alikiri kuutupa mwili wa mtoto kutokea kwenye paa hilohilo," msemaji wa polisi alivieleza vyombo vya habari vya nchini humo. "Hajakwepa kifo, lakini sasa ni kwa kupigwa risasi kwa kosa la kuua."
China ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya matukio ya kujiua duniani, ikiwekwa katika nafasi ya tisa katika orodha ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya matukio ya kujitoa mhanga.
Ikiwa na matukio 22.23 ya kujiua katika kila watu 100,000 yaliyoripotiwa mwaka 2010, China ina asilimia chache kuliko Latvia, Kazhakstan na Korea Kusini lakini jumla ya namba iko juu ya nchi nyingine kutokana na idadi kubwa ya watu iliyonayo.
WHO iliongeza kwamba orodha yao imeandaliwa kwa kutumia takwimu rasmi na imeegemea zaidi kwenye taarifa kutoka Jamhuri ya Watu wa China kuliko utafiti wao binafsi.
Mwaka jana Msemaji wa Shirika la Afya la Beijing, Mao Yu alithibitisha kuhusu majaribio zaidi ya milioni mbili ya kutaka kujiua kwa mwaka na kutangaza kwamba kujitoa mhanga ndio muuaji mkubwa zaidi kwa watu wa rika la kati ya miaka 15 hadi miaka 34.

No comments: