Watu wako kwenye semina ndipo wakaanza kujitambulisha kama ilivyo kawaida. Mmoja akasimama na kujitambulisha, "Naitwa Anna, niko mwaka wa kwanza Open University, nasoma Teknohama." Mwingine akasimama na kujitambulisha, "Naitwa Devi, niko mwaka wa tatu Mzumbe, nasoma Sheria." Ikafikia zamu ya jamaa mwingine kwa kusuasua akajitambusha, "Naitwa Cosmas, niko mwaka wa nne TANESCO, nasoma MITA!" Ukumbi mzima kicheko...

No comments:
Post a Comment