Mishahara katika sekta binafsi zinazoajiri Watanzania wengi wa kipato cha chini, ikiwamo watumishi wa majumbani, hoteli na ulinzi binafsi, inatarajiwa kuboreshwa baada ya Serikali kuandaa mazingira mazuri ya kuanza kupangwa kwa kima cha chini.
Tayari Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), imeshatoa mafunzo kwa wajumbe 89 wa Bodi 12 za mishahara ya kisekta watakaokuwa wanashughulikia upangaji wa kima cha chini cha mishahara katika sekta binafsi, ikiwemo kwa wafanyakazi hao kuanzia mwaka huu wa fedha.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka aliyasema hayo bungeni jana, alipokuwa anawasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa Fedha wa 2012/2013.
Wafanyakazi wengine ambao bodi zao zimeshapata mafunzo ya namna ya kupanga kima chao cha chini cha mshahara ni wafanyakazi wa ujenzi, mawasiliano, shule binafsi, madini, viwanda na biashara, afya, maji, hotelini, kilimo na usafirishaji.
Kutokana na hatua hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, imeipongeza Serikali kwa kuunda bodi 12 za mishahara ya kisekta, kwa lengo la kufanya tathmini na uchambuzi na hatimaye kutoa mapendekezo ya kima cha chini kwa sekta binafsi.
Pongezi hizo zilitolewa bungeni jana muda mfupi baada ya Waziri Kabaka kuwasilisha bajeti yake.
Akisoma maoni hayo kwa niaba ya kamati, mjumbe wake Assumpter Mshama ambaye pia ni Mbunge wa Nkenge (CCM), alisema ingawa Serikali imeahidi kufanya utafiti wa kima cha chini cha mshahara katika mwaka huu wa fedha, kamati inahimiza kazi hiyo kufanyika kwa umakini mkubwa na ikiwezekana ikamilike haraka.
Alisema uharaka wa kazi hiyo, utatoa suluhu ya malalamiko ya mishahara midogo kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na ile ya umma.
Alisema Kamati inashauri Serikali iangalie uwezekano wa kuruhusu uwepo wa viwango tofauti vya kima cha chini cha mshahara katika sekta moja baina ya wawekezaji binafsi wa ndani na wale wa kigeni.
Aliongeza kuwa, endapo utaratibu huo utaonekana kuwa na tija, wawekezaji wa kigeni waagizwe kulipa viwango vya juu vya kima cha chini ikilinganishwa na vile vinavyolipwa na wawekezaji wa ndani.
Kamati hiyo imepongeza kitendo cha madaktari na watumishi wa sekta ya afya kukubali kurejea kazini huku madai yao yaliyosababisha migomo mfululizo yakiendelea kushughulikiwa na mamlaka husika.
“Hatua hiyo inaonesha moyo wa kizalendo walio nao wataalamu hao hasa kwa kuzingatia kuwa taaluma yao ni muhimu kwa Taifa,” alisema.
Aidha, Kamati hiyo imewapongeza pia walimu kupitia Chama cha Walimu (CWT), kwa kutii uamuzi wa Mahakama na kurejea kazini.
Hata hivyo, imeelezea kusikitishwa kwake na utata uliojitokeza baina ya walimu na Serikali.
“Je, hakukuwa na mawasiliano ya kutosha baina ya Serikali na Chama cha Walimu kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya pande hizo juu ya madai ya walimu?” Alihoji.
Ili kumaliza tofauti baina ya pande hizo, kamati hiyo imewataka walimu na Serikali kurejea haraka katika meza ya mazungumzo ili kuhakikisha kuwa, suala la madai ya walimu linamalizwa kwa njia mwafaka bila ya kuifikisha nchi katika mgomo ambao mara nyingi huathiri watoto wa Watanzania wote.

No comments:
Post a Comment