Serikali baada ya kutafakari kwa kina, imekubali kuwasilishwa bungeni Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Malipo ya Mafao kwa Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Pamoja na mambo mengine, Serikali imefikia hatua hiyo ili kuondoa malalamiko yaliyokuwa yamejitokeza kwa wafanyakazi na wanachama wa mifuko hiyo baada ya sheria hiyo iliyopitishwa Aprili 13, mwaka huu kuanza kutekelezwa.
Taarifa hiyo ya Serikali ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.
Akizungumza baada ya kusoma takribani robo tatu ya makadirio ya wizara yake ya Sh bilioni 18.08, kati ya hizo Sh bilioni 13.1 zikiwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Waziri Kabaka alisema:
“Kabla ya kuhitimisha hoja yangu, naomba kutoa maelezo mafupi kuhusu Azimio la Bunge lililowasilishwa hapa jana (juzi) na Mheshimiwa Selemani Jafo, Mbunge wa Kisarawe (CCM) juu ya umuhimu wa kuletwa bungeni Muswada wa Dharura wa Marekebisho ya Sheria Namba Tano ya mwaka 2012 inayozungumzia marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ndani yake imeelezwa kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwa wafanyakazi.
“Sheria hii ilipoanza kutumika ilitafasiriwa kwa njia tofauti na hata vyombo vya habari viliripoti kwa njia tofauti. Wapo waliosema mifuko yetu inataka kufilisika na wengine wanasema mfumo huu umeanzishwa na CCM ili ipate fedha kwa ajili ya matumizi ya kisiasa.
“Hayo yote siyo kweli ila tatizo liliko hapa wakati mabadiliko haya yanakuja, hatukutoa elimu kwa wadau ndiyo maana malalamiko yamekuwapo.
“Katika hili namshukuru sana Mheshimiwa Jafo kwa sababu amezunguka katika migodi mbalimbali ikiwamo Geita, Bulyanhulu na Nyamongo ambako alizungumza na wafanyakazi.
“Kutokana na malalamiko kuwa mengi, Serikali imekubali kuleta muswada wa marekebisho ya sheria hiyo hapa bungeni ili ujadiliwe kwa undani na nasema mchakato wa muswada huu utapita hatua zote na tutatoa elimu kwa wadau ili waelewe.”
Uamuzi huo wa Serikali ulipokewa kwa vifijo bungeni, hali iliyoashiria kuwa wabunge wamefarijika na hatua hiyo, kwani tangu Jumanne ndani na nje ya Bunge walikuwa mbogo, wakilalamikia sheria hiyo inayozuia kujitoa katika mifuko ya hifadhi hadi mfanyakazi atakapofikisha umri wa kustaafu.
Kwa nyakati tofauti walisema, kuondoa fao la kujitoa ni kuwanyima haki wafanyakazi, ambao katika dunia ya sasa, wanafanya kazi katika mazingira tofauti.
Walitoa mfano wafanyakazi wa migodini wanaotajwa kuwa na nafasi ndogo ya kufikisha umri wa kustaafu kutokana na matumizi makubwa ya dawa na mionzi wakiwa kazini.
Aidha, walisema idadi kubwa ya wafanyakazi wameajiriwa katika sekta binafsi ambayo haitoi uhakika na ajira zao. Walihoji pia juu ya wanaofanya kazi kwa mikataba, bila ya kutaka kuendelea na ajira baada ya kumalizika kwa mikataba yao.
Kwa mujibu wa Waziri Kabaka, utaratibu wa wafanyakazi kujitoa na kuchukua mafao yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii, umekuwapo kwa muda mrefu na ulihusu wafanyakazi wote wa mikataba ya ajira ya masharti ya kudumu na malipo ya pensheni pamoja na wale wa mikataba ya masharti ya muda maalum.
Awali, msemaji wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM) alisema baada ya sheria hiyo kurekebishwa, mafao ya kujitoa yarejeshwe na pia wanachama waruhusiwe kutumia sehemu ya mafao yao ya uzeeni kulipia mkopo wa nyumba.
Aidha, Kamati ilitaka wanachama waruhusiwe kutumia sehemu ya mafao yao ya uzeeni kugharamia shughuli yoyote nyingine kwa lengo la kuandaa mazingira mazuri ya maisha baada ya kustaafu.
Kamati hiyo, ilipendekeza kupitiwa haraka na kufanyiwa marekebisho kwa sheria hiyo kwa kuzingatia mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na sheria kurejesha fao la kujitoa, mwanachama kuruhusiwa kutumia sehemu ya mafao yake ya uzeeni kulipia mkopo wa nyumba.
Aidha, imetaka wanachama waruhusiwe kutumia sehemu ya mafao yake ya uzeeni kugharimia shughuli yoyote nyingine kwa lengo la kuandaa mazingira mazuri ya maisha baada ya kustaafu.
Akichangia, Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Kawawa (CCM), aliitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA), ifanye kazi kwa uangalifu ili kuondoa malalamiko kwa wafanyakazi.
Michango yenye mtazamo huo ilitoka pia kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgallu (CCM) na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM).
Leo hakutakuwa na shughuli za Bunge kwa kuwa ni Sikukuu ya Nanenane na kesho itakuwa zamu ya Wizara ya Maendeleo na Mifugo na Uvuvi na Ijumaa na Jumamosi, itajadiliwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wiki ijayo ambayo itakuwa ya mwisho ya Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itajadiliwa Jumatatu na Jumanne wakati Jumatano itakuwa Wizara ya Fedha na Alhamisi itatumika kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha na kuahirisha Bunge.

No comments:
Post a Comment